2023
Ni kwa Jinsi Gani Utajiandaa Kwa Ajili ya Mkutano Mkuu
Septemba 2023


“Ni kwa Jinsi Gani Utajiandaa Kwa Ajili ya Mkutano Mkuu,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2023.

Kujiandaa kwa ajili ya Mkutano Mkuu

Ni kwa Jinsi Gani Utajiandaa Kwa Ajili ya Mkutano Mkuu

Vijana hawa walipata mengi kutoka kwenye mkutano mkuu. Unawezaje kujiandaa kuwa na uzoefu wenye maana?

Ninataka kumfuata Nabii

Picha
mvulana

Nilijiandaa kwa ajili ya mkutano mkuu wa Oktoba 2022 kwa kusoma kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo katika kitabu cha Mormoni na katika Agano la Kale.

Wakati wa mkutano mkuu, Rais Russell M. Nelson alizungumza nasi na alishuhudia kuhusu umuhimu wa hekalu.1 Ndani ya hekalu, baraka za milele zinaahidiwa, na roho nzuri huhisiwa unapokuwa pale.

Bado hakuna hekalu Nicaragua, lakini moja limetangazwa karibuni. Natumaini Ninaweza kusikiliza maneno ya Rais Nelson na kwenda hekaluni pale litakapo malizika.

Nilipokuwa naangalia mkutano mkuu, Nilimhisi Roho akishuhudia kwamba nilikuwa sehemu sahihi. Nilihisi kama moyo wangu ulikuwa umejawa na upendo wa Mungu.

Carlos M., Nicaragua

Uponyaji Unapatikana kwa Wote

Picha
msichana

Kabla ya mkutano mkuu mnamo Oktoba 2022, nilitafakari juu ya mambo ambayo yametokea katika maisha yangu hivi karibuni. Mambo mengi yalikuwa yanasumbua akili yangu kabla ya mkutano mkuu, na nilitaka kuhisi faraja, amani, na nguvu.

Wakati wa mkutano mkuu, Mzee Quentin L. Cook wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema, “Kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi, uponyaji Unapatikana kwa Wote.”2

Maneno hayo yalinipa amani na tumaini. Kupitia upatanisho wa Yesu Kristo, ninapofanya makosa na chaguzi hasi ninaweza kusamehewa na kuhisi amani. Na maumivu yoyote ninayoweza kuyasikia, ninaweza kuponywa. Sisi sote tunaweza kuhisi amani na uponyaji ule ule tunapotubu dhambi zetu na kujitahidi kuwa wema kila siku.

Kaye D., Ufilipino

Maandalizi yako ya mkutano mkuu

Chukua muda kiasi kujiandaa kwa ajili ya mkutano mkuu, na utakuwa na uzoefu mzuri zaidi. Kwa hiyo, unajiandaaje? Anza kwa kuandika maswali yako! Tafakari maswali yako wakati unapotazama, na utashangazwa kwa namna ambavyo mara nyingi wazungumzaji wanaonekana kuzungumza na wewe moja kwa moja.

Chapisha