2023
Unahisi Mfadhaiko, Wasiwasi au Huzuni?
Septemba 2023


“Unahisi Mfadhaiko, Wasiwasi au Huzuni?,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Sep. 2023.

Msaada wa Kimaisha

Unahisi Mfadhaiko, Wasiwasi au Huzuni?

Haya ni mambo unayoweza kufanya.

Kifaa chenye rangi tofauti tofauti na mwonekano tofauti tofauti wa sura.

Kipimo cha Mfadhaiko

Unahisi huzuni au mfadhaiko kiasi gani?

Kama unapitia kutokuwa na tumaini, mfadhaiko au wasiwasi wa muda mrefu, tafadhali tafuta msaada kwa kuzungumza na mtu mzima unayemwamini. Ungeweza pia kujaribu ushauri katika sehemu za njano (hususani mambo ya msingi!), lakini wakati mwingine unaweza kuhitaji msaada zaidi, na hilo ni SAWA.

Kama unahisi kutaka kujiua, pata msaada mara moja. Wasiliana kwa simu ya dharura ya eneo lako, idara ya polisi, au hospitali.

Ni kawaida wakati fulani kuwa mwenye wasiwasi, mwenye huzuni, au kuwa na mfadhaiko. Hisia hizi mara nyingi zinachokonolewa na hali ya maisha na huja na kuondoka kadiri maisha yanavyobadilika. Jaribu baaadhi ya ushauri ambao unaweza kusaidia!

Mambo ya Msingi

  • Mgeukie Baba wa Mbinguni. Yeye anasikia na kujibu sala zako. Atakusaidia ukabiliane na changamoto ambazo hukujia.

  • Fokasi juu ya Kristo. “Furaha tunayoihisi inahusika kwa kiasi kidogo na hali ya maisha yetu na inahusika na kila kitu kinachohusu fokasi ya maisha yetu.”1

  • Watumikie wengine. “Tunapojikita kwenye kuwahudumia wengine, tunagundua maana ya maisha na furaha yetu wenyewe.”2

  • Fanya roho yako iwe na afya. Soma maandiko kila siku, hudhuria hekaluni pale inapowezeka, shiriki sakramenti, tii maagano yako, na tubu kila siku. Omba baraka za ukuhani pale unapozihitaji.

  • Tunza afya ya mwili wako. Pata usingizi wa kutosha na mazoezi na tii Neno la Hekima.

Kama Unahisi wasiwasi

  • Fokasi kwenye usahihi sasa. Haisaidii kuwa na wasiwasi kuhusu baadaye au kufadhaika kuhusu yaliyopita. Muda uliopo ndiyo kitu pekee ambacho kiuhalisia unaweza kubadili.

  • Ondoa wasiwasi. “kwani haimpasi mwanadamu kukimbia zaidi kuliko nguvu zake” (Mosiah 4:27).

  • Kuwa na mawazo chanya. Hisia hasi zinaweza kusababishwa na mawazo hasi. Fikira chanya zinaweza kukusaidia uhisi woga au wasiwasi kidogo.

Kama Unahisi Huzuni

  • Jua kwamba majaribu ni sehemu ya mpango. Kupitia hali ngumu si lazima kumaanishe kwamba unafanya chochote kibaya. Amini kwamba Baba wa Mbinguni atakuimarisha na kwamba changamoto zako zitafanyika kwa pamoja kwa ajili ya faida yako (Mafundisho na Maagano 90:24; (ona pia Warumi 8:28; Mafundisho na Maagano 122:5–9).

  • Fokasi kwenye shukrani. Andika vitu ambavyo kila siku una shukrani kuvihusu , na hakikisha unamshukuru Baba wa Mbinguni (ona Mafundisho na Maagano 98:1).

  • Fanya vitu ambavyo hukupa furaha. Tumia muda na marafiki na familia, jaribu jambo jipya , sikiliza muziki wa kutia moyo, au panga shughuli za kuburudisha.

Kama Hauhisi Kwamba Unafaa vya Kutosha

  • Jua kwamba huhitaji kuwa mkamilifu. “Katika maisha haya ukamilifu bado ‘una ngoja.’”3 Usijilinganishe na wengine, iwe kwenye maisha yako halisi au kwenye mitandao ya kijamii.

  • Jizungumzie kwa upole. Kuwa mkarimu kwa nafsi yako, kama vile ambavyo ingekuwa kwa rafiki yako. Roho Mtakatifu pia atazungumza nawe kwa upole na kamwe hatakudhihaki au kukudhalilisha.

  • Jua kwamba Mwokozi anafidia tofauti. Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na alijichukulia maumivu yetu, magonjwa, na udhaifu (ona Alma 7:11-12). Kama tukiwa wanyenyekevu, Ameahidi “kufanya vitu dhaifu kuwa vyenye nguvu” (Etheri 12:27). Tunaweza kuwa sio wazuri vya kutosha , lakini tunaweza kuwa wazuri vya kutosha pamoja Naye.

Hitimisho

Unaweza pengine kuwa na siku nyingi unapohisi kujiamini na tayari kukabiliana na changamoto za maisha. Bila kujali ni kwa kiasi gani unahisi vizuri, hakikisha unaendelea kufanya mambo ya msingi.

Omba kwa Baba wa Mbinguni—hata wakati maisha ni rahisi. Fokasi kwenye kile ambacho Mwokozi amefanya kwa ajili yako na kwenye maisha na mafundisho Yake—hata wakati ambapo mambo yanakwenda vizuri. Kisha wakati unapitia hisia za ugumu, utakuwa umejitayarisha vyema kuzikabili.