2023
Kwa nini tunahitaji kufanya ubatizo kwa niaba ya mababu waliokufa?
Septemba 2023


“Kwanini tunahitaji kufanya ubatizo kwa niaba ya mababu waliokufa?,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2023.

Kwenye Hoja

Kwa nini tunahitaji kufanya ubatizo kwa niaba ya mababu waliokufa?

Picha
wavulana akiwa na vipande vya karatasi mbele ya hekalu

Yesu Kristo alifundisha kwamba watu wote lazima wabatizwe ili kuingia ufalme wa Mungu baada ya maisha haya (ona Yohana 3:5) Lakini watu wengi hawakuweza kamwe kupata fursa hiyo.

Mungu amefunua kwamba wale waliofariki ambao hawakubatizwa wanaweza kupata injili ya Yesu Kristo kuhubiriwa kwao katika ulimwengu wa roho (ona 1 Petro 3:18–19; Mafundisho na Maagano 138:30–33). Pia Amefunua kwamba walio hai wanaweza kubatizwa kwa niaba ya watu hawa (ona 1 Wakorintho 15:29; Mafundisho na Maagano 124; 128). Ubatizo huu lazima ufanyike hapa duniani.

Tunaweza kutafuta kumbukumbu za mababu waliofariki na kufanya ubatizo kwa niaba yao katika mahekalu. Hii huwapa wao fursa ya kukubali ubatizo, ambao ni muhimu kwa ajili ya ufalme wa selestia.

Mzee D. Todd Christofferson amesema: “Juhudi zetu kwa niaba ya waliofariki zinatoa ushuhuda mzuri kwamba Yesu Kristo ni Mkombozi mtakatifu wa wanadamu wote. Neema yake na ahadi zinawafikia hata wale ambao katika uhai hawampati Yeye” (Mkutano mkuu wa Okt 2000 [Ensign, Nov. 2000, 11).

Chapisha