2023
Muda wa Dansi
Septemba 2023


“Muda wa Dansi,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Sept. 2023.

Muda wa Dansi

Vijana hawa walipata furaha kupitia kushinda woga na kushiriki vipaji vyao na wengine.

wavulana na wasichana wakidansi

Picha na Cristy Powell

Emo’onahe Y. Mwenye umri wa miaka kumi na minne na Jax C. Wana angalau kitu kimoja kinachowaunganisha: Wote wawili kwa kawaida walicheza dansi kwenye mkutano wa maonyensho mbalimbali ya KNV huko Provo, Utah.

Kucheza peke yake mbele ya maelfu ya vijana haikuwa rahisi kwa yoyote kati yao. Lakini walipotafuta kujiendeleza na kushiriki vipaji vyao, wamepokea ufunuo na kuweza kukua katika njia ambazo zime wasaidia “kuwa zaidi kama Yesu Kristo, na kuwafanya wao [wenyewe], watu wengine, na hata ulimwengu kuwa bora” (Personal Development: Youth Guidebook [2019], 1).

Kudansi mduara na Emo’onahe

Emo’onahe (eh-moh-oh-nah) aliamua kushiriki kipaji chake cha kudansi mduara, ambao ni sehemu ya utamaduni wake wa wenyeji wa Marekani. “Mmoja kati ya rafiki zangu aliyekwenda KNV kabla yangu aliniambia kwamba walikuwa na maonyesho ya kipaji cha aina hii na kwamba ninapaswa kukionesha,” alisema.

“Nilikuwa na wasiwasi kidogo kwa hiyo nilijaribu kutokufokasi kwenye umati.” Lakini haikuwa rahisi! “Niliweza kusikia kila mtu akipata hisia kali” alisema. “Walikuwa na kelele nyingi sikuweza hata kusikia muziki vizuri, kwa hiyo kwa shida niliweza kufuata mapigo ya muziki.

Emo’onahe ameweza kufanya kazi kubwa kuweza kuwa mzuri katika kudansi mduara. Anasema, “Kulikuwa na kazi ngumu ya kujifunza.” Lakini kadiri alivyofanya mazoezi, ndivyo alivyojifunza kuhusu yeye mwenyewe.

picha za msichana anayefanya dansi za Wenyeji wa Marekani

Mwenye kipaji cha Kusimulia hadithi

Dansi ya mduara ni aina ya kusimulia hadithi binafsi. “Unaanza na mduara mmoja kuwakilisha mwanzo wako, na kisha unaendelea kuongeza miduara kuonesha mambo zaidi kuhusu maisha yako. Katika uwasilishaji wangu, ungeweza kuona kipepeo, tai, na mchunga ng’ombe,” Emo’onahe anasema. “Ninaposimulia hadithi yangu, nahisi kama ninasimulia hadithi ya wale niliojifunza kutoka kwao na uzoefu nilioupata.”

Emo’onahe ni wa kutoka makabila ya Cheyenne na Arapanne ya Oklahoma, na pia ni Fork Peck Sioux na Assiniboine. Anaeleza , “Nilikuwa nikijihisi tofauti kabisa na wengine wote,” na wakati mwingine “hiyo ilinifanya nikose raha.” Lakini dansi ya mduara inakumbatia nafsi. Kila mchezaji anaumba miondoko yake ya dansi, na “hiyo ndiyo inaifanya iwe ya kipekee mno na ya binafsi kwako,” anasema.

Vipaji Vinaweza Kuimarisha

Emo’onahe anahisi kuwa karibu mno na Mungu pale anaposali, anaposoma maandiko, na kujitahidi kumfuata Yesu Kristo. Pia anajihisi karibu mno na Mungu pale anapojitahidi kuboresha vipaji vyake. “Ninapochukua miduara yangu na kudansi, ninaweza kuhisi furaha.” Anapendekeza: “Tafuta vitu unavyovipenda na tafuta watu wazuri watakaokusaidia ili uweze kutumia vipaji vyako kujiimarisha wewe mwenyewe na wengine. Kuwahudumia wengine kunaweza vilevile kukusaidia uimarishe ushuhuda wako wa Yesu Kristo.”

Dansi ya Kiairishi na Jax

Jax alikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kuonesha kipaji chake, dansi ya Kiairishi kwenye maonyesho mbalimbali ya KNV. “Kwa kweli nilikuwa na hofu, hofu sana. Kama vile nilikuwa sehemu ya kutisha ya kuogofya,” anasema. “Nilisali kabla sijapanda jukwaani. Nilikuwa bado nina hofu, lakini muziki ulianza. Nilijifanya kama vile hakukuwa na yoyote pale. Na nilianza kudansi.”

Jax aliruka na kuhamisha miguu yake katika utamaduni na mtindo wa kiairishi. Lakini kuangalia uso wa Jax wenye furaha, watu wengi pengine wasingekisia kwamba ilikuwa ni safari ndefu kwa yeye kuwa pale.

picha za mvulana anayecheza dansi ya kiairishi

Kukuza Kipaji Husaidia kudhibiti Msongo wa mawazo

“Mnamo mwaka 2020 kiukweli nilikuwa na msongo wa mawazo na hata karibu kujiua,” Jax anaeleza. Nilipelekwa kwenye hospitali ya afya ya akili kwa mwezi mzima. Niligundua nilikuwa na uvimbe kwenye ubongo na kugundua kuwa nilikuwa na aina ya ugonjwa wa akili. “Kwa kweli ilikuwa vigumu, vigumu sana kwangu.”

Baada ya Jax kupokea baadhi ya matibabu kwa ajili ya afya ya akili yake, mama yake alimtia moyo kutafuta shughuli ya kimwili itakayomsaidia kudhibiti msongo wa mawazo. Aliamua kutafuta ufunuo binafsi kuhusu nini angeweza kufanya.

“Nilisali kuhusu hilo na niliomba kwa ajili ya msaada,” anaeleza. “Na nilikumbuka kwamba shangazi yangu alikuwa anafundisha dansi ya Kiairishi. Kwa hiyo nilianza darasa mara moja kabla ya maonyesho yetu makubwa ya Krismasi. Ilibidi nijifunze aina kama tano za dansi ndani ya wiki mbili, kwa hiyo ilikuwa burudani,” Jax anatania. Punde, dansi ya Kiairishi ilikuwa baraka kubwa katika maisha yake. “Kwa kweli ilisaidia katika kudhibiti msongo wangu wa mawazo na hisia za giza,” anasema.

Kushiriki Kipaji chake

Kwenye KNV, Kombania ya Jax ilimwuliza kama alikuwa na kipaji ambacho angeweza kushiriki katika maonyesho. Hivyo alidansi pembeni ya njia kwa ajili yao. Walipomwambia anapaswa kufanya onyesho, wazo la kwanza lilikuwa, “Oh hapana.” Lakini aliamua kushiriki kipaji chake hata kama alikuwa anaogopa.

Sasa kwa vile Jax ameshaona video zake mwenyewe akicheza kwenye KNV hubaki tu akicheka. “Nilikuwa na uso mkavu kwenye sehemu ya kwanza,”anasema. “Lakini kisha watu walianza kushangilia, na nilianza kutabasamu.”

Kwa vijana ambao wanasumbuka, Jax anatoa ushauri huu: “Ni vyema kuzungumza kuhusu hilo na mtu fulani kuliko kuficha kama alivyofanya yeye. Bwana anajua wewe ni nani, na Atakuwa pale kwa ajili yako. Bwana anataka kukusaidia.”

Kwa ujumla, Jax anahisi kwamba kujifunza dansi ya Kiairishi kumekuwa baraka kutoka Baba wa Mbinguni.

msichana na mvulana wakidansi

Wewe ni wa kipekee.

Huwezi jua—wakati wewe unapomgeukia Bwana, pengine utashawishika kujenga kipaji kipya, pia.

Kama vile Emo’onahe na Jax, Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia utambue vipaji. Unapokuza vipaji hivi na kuvishiriki, unaweza kupata msaada pale unapojitahidi kuwa zaidi kama Mwokozi.

Ni vipaji gani unaweza kukuza na kushiriki?