2023
Kuchagua Kuhudumia
Septemba 2023


“Kuchagua Kuhudumia,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2023.

Nayaweza Mambo Yote katika Kristo

Vijana wanashiriki jinsi Kristo alivyowaimarisha wafanye mambo magumu (ona Wafilipi 4:13).

Kuchagua Kuhudumia

mvulana

Siku zote nilitaka kuhudumu misheni, lakini nilipokuwa na umri wa miaka 18 janga la ulimwenguni kote lilianza. Sikuhisi utayari wa kuhudumu, kwa hiyo nilianza chuo, na nilipata udhamini mkubwa wa elimu. Watu wengi walipendekeza kwamba nisingepaswa kwenda kuhudumu misheni. Nilihisi kama nilikuwa napoteza tamanio langu la kuhudumu.

Lakini kwenye mkutano mkuu Rais M. Russell Ballard alisema, “Kama bado upo kwenye umri wa kuhudumu kama mmisionari lakini bado hujafanya hivyo kutokana na janga la ulimwenguni kote au sababu zingine, ninakualika ufanye hivyo sasa.”1 Aliposema neno “sasa,” nilihisi kama vile alikuwa anasema na mimi—kwamba mimi lazima nitumikie misheni sasa. Tangu siku ile nilisali kuhusu hilo na nilipokea uthibitisho kwamba ni muda muafaka kwa mimi kumtumikia Bwana.

Nimepokea ukosoaji mwingi kuhusu uamuzi wangu. Hata udhamini wangu wa elimu ulifutwa. Lakini tamanio langu kwenda lina nguvu ya kutosha kiasi kwamba hakuna kati ya vitu hivyo vina maana zaidi kwangu. Niliitwa kuhudumu Misheni ya Guatemala Quetzaltenango. Ni maalumu mno kwa sababu wazazi wangu waliunganishwa kwa milele yote huko Guatemala.

Kama unajiuliza ikiwa unapaswa kuhudumu misheni, bado hujachelewa sana! Siku zote tumainia katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Watatuongoza na kutubariki kwa vitu ambavyo hatuwezi kufikiria.

Enoc M., Jamhuri ya Dominika