2023
Manabii Wanawafuata Manabii
Septemba 2023


“Manabii Wanawafuata Manabii,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2023.

Kujiandaa kwa ajili ya Mkutano Mkuu

Manabii Wanawafuata Manabii

Mtu yeyote anaweza kupata baraka kwa kumfuata nabii—hata Mitume.

Daima tunaaswa kumfuata nabii. Lakini baadhi wanaweza kushangazwa kwa nini sauti ya nabii ni muhimu mno kuifuata.

Mnamo mkutano mkuu wa Aprili 2017, Rais Thomas S. Monson, nabii wa wakati huo, aliwaomba waumini wa Kanisa wajifunze Kitabu cha Mormoni , na si tu kukisoma kila siku. Rais Russell M. Nelson na Rais Henry B. Eyring wote wawili walifuata ushauri wa nabii na walizungumza kuhusu kile kilichotokea.

Mtume Mtiifu

Picha
Russell M. Nelson

Rais Nelson alisema: “Nimejaribu kufuata ushauri [wa Rais Monson]. Miongoni mwa vitu vingine, nimeweka orodha ya Kitabu cha Mormoni ni nini, kinathibisha nini, kinakanusha nini, kinatimiza nini, kinafafanua nini na nini kinafunua. Kuangalia Kitabu cha Mormoni kupitia lenzi hizi imekuwa ni zoezi la umaizi na msukumo!”1

Rais Nelson aliendelea kueleza kwamba aliwauliza wengine maswali yaleyale na kupata kwamba maisha mengi mno yameguswa kwa kufuata ushauri wa Rais Monson. Bwana hutuongoza sote kupitia nabii wetu, maandiko, na ufunuo binafsi.

Mtume Mtiifu

Picha
Henry B. Eyring

Rais Eyring alisema: “Nimesoma Kitabu cha Mormoni kila siku kwa zaidi ya miaka 50. Kwa hiyo pengine ningeweza kufikiri kimantiki kwamba maneno ya Rais Monson yalikuwa kwa ajili ya mtu mwingine. Hata hivyo, Kama wengi wenu, Nilihisi hamasa kutoka kwa Nabii na ahadi yake ikinialika kufanya bidii zaidi.”

Rais Eyring aliendelea: “Kusikiliza ushauri wa Rais Monson kumekuwa na matokeo mengine mawili ya ajabu kwangu: Kwanza, Roho aliyoahidi imetoa hisia ya tumaini kuhusu kile kilichoko mbele, hata wakati mtafaruku ulimwenguni unapoonekana kuongezeka. Na, pili, Bwana amenipa mimi—na wewe—hisia kubwa zaidi ya upendo wake kwa wale walio katika dhiki.”2

Kila Mtu

Kila mtu anaweza na anapaswa kufuata ushauri wa nabii kutoka kwenye mkutano mkuu. Bila kujali uko wapi kwenye safari yako ya kiroho, unaweza siku zote kujiboresha, iwe wewe ni mtume, mwongofu mpya, au popote katikati ya hao. Haipunguzi uhitaji wetu kwa ajili ya ufunuo binafsi, ni njia nyingine ambayo Mungu anaweza kutubariki. Kama hata Mitume wanaweza kupata baraka za ziada kwa njia hii, sisi sote tuliobaki kwa hakika tunaweza pia.

Chapisha