2023
Sasa Kristo Amefufuka
Septemba 2023


“Sasa Kristo Amefufuka,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Sept. 2023

Mstari juu ya Mstari

Sasa Kristo Amefufuka

Jifunze kuhusu kile Mtume Paulo alichofundisha kuhusu Kufufuka kwa Yesu Kristo.

Picha
Yesu Kristo aliyefufuka

Kristo Aliyefufuka, na Wilson J. Ong

Sasa Kristo Amefufuka kutoka kwa wafu

Yesu Kristo alikufa msalabani, alilazwa kaburini, na akafufuka kutoka wafu siku ya tatu.

Malimbuko yao waliolala

Neno la Kiyunani lililotumika hapa kwa malimbuko linamaanisha zao la mwanzo kabisa la mwaka. Ni la kwanza kuvunwa —la kwanza kwa mengi zaidi yanayokuja.

Kirai wale ambao wamelala kinamaanisha “hao ambao wamekufa.”

Yesu Kristo alikuwa wa kwanza kufufuka, na, baada ya Ufufuko Wake watu wote watafufuliwa.

Kupitia mwanadamu kifo kilikuja

Hii ni kuzungumza kuhusu Adamu. Kuanguka kwake kulimaanisha kwamba watu wote watakao kuja ulimwenguni watakufa. (Ona Musa 4.)

Katika Kristo wote watafufuliwa

Kwa sababu ya Ufufuko wa Yesu Kristo, watu wote watafufuliwa. Hiyo inamaanisha kwamba kila mtu ambaye wakati wowote aliishi au wakati wowote ataishi atafufuliwa. Roho zetu zitaungana tena na miili yetu, na miili yetu itakuwa iliyo kamili na isiyokufa. (Ona Alma 11:43–45.)

Chapisha