2023
Kutoka Waraka hadi Mitiririko ya Moja kwa Moja
Septemba 2023


“Kutoka Waraka hadi Mitiririko ya Moja kwa Moja,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Agosti 2023.

Kujiandaa kwa ajili ya Mkutano Mkuu

Kutoka Waraka hadi Mitiririko ya Moja kwa Moja

Mawasiliano kutoka kwa viongozi wa Kanisa yameanza zamani sana, lakini malengo yanabaki yaleyale.

Picha
Paulo akiandika waraka

Takribani miaka 2,000 Iliyopita

Wakati alipokuwa duniani, Yesu Kristo alianzisha Kanisa Lake. Baada ya Mwokozi kufufuka na kupaa mbinguni, Mitume Wake waliongoza Kanisa kwa mamlaka, ufunuo, na msukumo ambao Yeye aliwapa.

Katika siku hizo, viongozi wa Kanisa mara nyingi waliwasiliana na waumini wa Kanisa katika maeneo mbalimbali kupitia nyaraka (barua).

Agano Jipya limejaa barua zilizoandikwa na Paulo, Petro, Yohana, Yakobo, na Yuda. Barua hizi ziliandikwa kwa mkono, kuwasilishwa kwa mkono, kunakiliwa kwa mkono na kusomwa kwa sauti kubwa.

Viongozi hawa wa Kanisa mara nyingi walikuwa na azma zinazofanana katika kuandika barua hizi. Walitafuta:

  • Kutoa ushuhuda na kufundisha Injili ya Yesu Kristo.

  • Kuhimiza, kutia moyo, na kuinua.

  • Kukumbusha juu ya amri na maagano.

  • Kushughulikia changamoto zilizopo.

  • Kutoa tahadhari ya hatari.

  • Kusahihisha makosa yoyote ambayo yaweza kuwa yaliingia katika Kanisa.

  • Kuliunganisha Kanisa.

Picha
Russell M. Nelson

Leo

Kwa haraka ukienda mbele takribani miaka 2,000 utaona kwamba mambo mengi yamebadilika, lakini baadhi ya mambo bado yako vilevile.

Yesu Kristo amerejesha Kanisa Lake duniani, na kuna manabii na mitume wa kuliongoza tena. Lakini tangu siku za nyaraka, teknolojia ya mawasiliano imepiga hatua—kutoka mashine ya kupiga chapa mpaka redio mpaka runinga mpaka intaneti.

Viongozi wa kanisa wanaweza sasa kutoa jumbe kwenye mkutano mkuu kwa ajili ya Kanisa lote kwa mara moja. Zinapelekwa hata kwenye satelaiti na kurushwa moja kwa moja kwenye mtandao katika lugha kadhaa kwa wakati mmoja. Ndani ya siku kadhaa, maandishi yanawekwa kwenye mtandao katika lugha tofauti tofauti na nakala zilizochapishwa hutumwa ulimwenguni kote.

Unapojiandaa kwa ajili ya mkutano mkuu unaokuja, unaweza kufikiria kuhusu barua hizo za Agano Jipya. Hizo zilikuwa nyakati tofauti, na teknolojia zilikuwa tofauti sana. Lakini jumbe za mkutano mkuu zinakamilisha azma zilezile muhimu. Unapopata uzoefu wa jumbe za mkutano mkuu, unaweza kufikiri kuhusu jinsi zinavyoweza:

  • Kutoa ushuhuda na kufundisha Injili ya Yesu Kristo.

  • Kuhimiza, kutia moyo, na kuinua.

  • Kukumbusha juu ya amri na maagano.

  • Kushughulikia changamoto zilizopo.

  • Kutoa tahadhari ya hatari.

  • Kusahihisha makosa yoyote ambayo yaweza kuwa yaliingia katika Kanisa.

  • Kuliunganisha Kanisa.

Chapisha