2023
Ninaweza Kukaa Ndani ya Mistari
Septemba 2023


“Ninaweza Kukaa Ndani ya Mistari,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Sept. 2023.

Nayaweza Mambo Yote katika Kristo

Vijana wanashiriki jinsi Kristo alivyowaimarisha wao kufanya vitu vigumu (ona Wafilipi 4:13).

Ninaweza Kukaa Ndani ya Mistari

Picha
msichana akikimbia katika uwanja wa mbio za miguu

Tangu nilipoanza kukimbia katika uwanja wa mbio za miguu, imekuwa ndoto yangu kuvunja rekodi ya shule katika mbio za maili moja. Kisha kuelekea mwisho wa msimu huu nilikimbia maili moja ndani ya dakika tano kamili, nikivunja rekodi kwa zaidi ya sekunde tatu.

Siku iliyofuata, hata hivyo, tuligundua kwamba maili yangu haikuhesabiwa. Maafisa wenye mamlaka walieleza kwamba nilikuwa hatua tatu mbele ya mstari, ambayo iliniondolea ustahili kwenye shindano la mbio. Kocha wangu alibisha kwamba hiyo ilitokana na mimi kusukumwa na mkimbiaji mwingine. Afisa alisema, “yawezekana haikuwa kosa lake kwamba alisukumwa, lakini lilikuwa kosa lake kwamba alikuwa karibu mno na mstari.” Niliondoka nikihisi kama mafanikio yangu yalikuwa yameondolewa kimakosa.

Jumapili iliyofuata katika darasa la wasichana tuliangalia video ambayo ilifananisha kubaki katika mistari katika michezo na utiifu wa amri.1 Muda wote wa somo nilikaa pale, nikiwa na hasira kwa ukumbusho kwamba nilikuwa nimeshindwa.

Siku iliyofuata nilipokuwa nakimbia uwanjani, nilitazama chini na niligundua nilikuwa nakimbia sahihi ndani ya mstari. Na kila mara wakati fulani, nilikanyaga ndani ya mstari, kama vile afisa alivyokuwa amesema. Mara moja niliacha kukimbia, nikiwa nimenyenyekezwa. Nilikuwa sina wasiwasi kabisa juu ya sehemu ambayo nilikuwa nakimbilia kiasi kwamba sikuweza kuona hatari yoyote.

Kwa bahati nzuri nilipewa nafasi ya pili wiki chache baadaye. Nilijiweka mbali na mstari na nilivunja rekodi ya shule, wakati huu nikiwa ndani ya mipaka.

Uzoefu ule ulinifanya nitafakari kuhusu ukimbiaji wangu wa karibu na mstari linapokuja suala la amri. Lakini kwa sababu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake, siku zote napewa nafasi nyingine pale ninapotubu.

Linapokuja suala la amri, tunapaswa kujiweka mbali na mstari na kufanya kadiri tuwezavyo kubakia kwenye mipaka. Lakini nina shukurani kwamba tunapofanya makosa, Mwokozi anaturuhusu tutubu na tujaribu tena.

Raygan P., Utah, Marekani

Muhtasari

  1. Ona Jeffrey R. Holland, “Stay within the Lines” (youth video), ChurchofJesusChrist.org.

Chapisha