Maamuzi ya Milele
Matumizi ya hekima ya uhuru wako wa kufanya maamuzi yako mwenyewe ni muhimu kwa ukuaji wako wa kiroho sasa na kwa milele.
Wapendwa ndugu na dada zangu, kila siku ni siku ya uamuzi. Rais Thomas S. Monson ametufundisha kwamba “maamuzi huamua kudura.”1 Matumizi ya hekima ya uhuru wako wa kufanya maamuzi yako mwenyewe ni muhimu kwa ukuaji wako kiroho, sasa na kwa milele. Wewe kamwe si mchanga sana kujifunza, si mzee sana kubadilika. Mapenzi yako ya kujifunza na kubadilika huja kutokana na hamu ya kujitahidi takatifu iliyotolewa kwa ukuaji wa milele.2 Kila siku huleta fursa ya maamuzi ya milele.
Sisi ni viumbe vya milele —watoto wa kiroho wa wazazi wa mbinguni. Biblia inaandika kwamba “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, …mwanaume na mwanamke aliwaumba.”3 Hivi majuzi nilisikia sauti ya watoto wakiimba wimbo niupendao “Mimi ni Mtoto wa Mungu.”4 Nilishangaa, “Ni kwa nini sijasikia wimbo huo unaoimbwa mara nyingi zaidi na kina mama waimbaji au kina baba waaminifu?” Je, si sisi sote ni watoto wa Mungu? Kwa kweli, hakuna mmoja wetu anayeweza kukoma kuwa mtoto wa Mungu!
Kama watoto wa Mungu, tunapaswa kumpenda kwa moyo wetu wote na nafsi, hata zaidi tunavyopenda wazazi wetu wa duniani.5 Tunapaswa kuwapenda majirani zetu kama ndugu na dada. Hakuna amri zingine ambazo ni kubwa kuliko hizi.6 Na lazima daima tuheshimu thamani ya maisha ya binadamu, kupitia kwa kila moja ya hatua zake nyingi.
Maandiko yanafundisha kwamba mwili na roho ni ndiyo nafsi ya mwanadamu.7 Kama kiumbe wa sehemu mbili, kila mmoja wenu anaweza kumshukuru Mungu kwa zawadi Zake zenye thamani za mwili wako na roho yako.
Mwili wa Binadamu
Miaka yangu ya kitaalamu kama daktari wa matibabu ilinipa heshima kubwa kwa mwili wa binadamu. Uliumbwa na Mungu kama zawadi kwako, ni ajabu kabisa! Fikiria juu ya macho yako yanayoona, masikio yanayosikia, na vidole vinavyohisi vitu vyote vya ajabu karibu nawe. Ubongo wako unakuwezesha kujifunza, kufikiri, na kuamua. Moyo wako unapiga bila kuchoka mchana na usiku, hata bila kujua kwako.8
Mwili wako hujikinga wenyewe. Maumivu huja kama onyo kwamba kuna kitu ambacho si sawa na kinahitaji kuangaliwa. Magonjwa ya kuambukiza yanatokea mara kwa mara, na yanapotokea, kingamwili zinajengwa zinazoongeza kinga yako dhidi ya maambukizi ya baadaye.
Mwili wako hujirekebisha wenyewe. Majeraha na michubuko hupona. Mifupa iliyovunjika inaweza kuwa na nguvu mara nyingine tena. Nimetoa lakini sampuli kidogo tu za mfano sifa za kushangaza zilizotolewa na Mungu kwa mwili wako.
Hata hivyo, inaonekana kwamba, katika kila familia, kama si katika kila mtu, hali fulani ya kimwili zipo ambazo zinazohitaji utunzaji maalum.9 Njia ya kukabiliana na changamoto hizo zimepeanwa na Bwana. Yeye alisema, “ninawapa watu udhaifu ili katika udhaifu wao wawe wanyenyekevu; … kwani wakijinyenyekeza mbele yangu …na kuwa na imani ndani yangu, ndipo, nitafanya vitu dhaifu kuwa vya nguvu kwao.”10
Roho maalumu mara nyingi zinapatikana katika miili dhaifu.11 Zawadi ya mwili kama hiyo inaweza kwa kweli kuimarisha familia kama wazazi na watoto wanapojenga maisha yao kwa hiari kumzunguka yule mtoto aliyezaliwa na mahitaji maalum.
Mchakato wa kuzeeka pia ni zawadi kutoka kwa Mungu, kama vile kifo. Kifo cha hatima ya mwili wako ni muhimu kwa mpango mkuu wa Mungu wa furaha.12 Kwa nini? Kwa sababu kifo kitaruhusu roho yako kurudi nyumbani Kwake.13 Kutokana na mtazamo wa milele, kifo tu ni cha mapema kwa wale ambao hawako tayari kukutana na Mungu.
Na mwili wako ukiwa sehemu muhimu ya mpango wa Mungu wa milele, si ajabu kwamba Mtume Paulo aliielezea kama “hekalu la Mungu.”14 Kila wakati unapoangalia katika kioo, ona mwili wako kama hekalu lako. Kweli hiyo ikiwekwa upya kila siku kwa shukrani---inaweza kushawishi maamuzi yako vyema kuhusu jinsi unavyoweza kutunza mwili wako na jinsi utautumia. Na maamuzi hayo yataamua hatima yako. Hii inawezekanaje? Kwa sababu mwili wako ni hekalu la roho yako. Na jinsi unavyotumia mwili wako huathiri roho yako. Baadhi ya maamuzi ambayo yataamua hatima yako ya milele yanajumuisha:
-
• Utawezaje kuchagua kutunza na kutumia mwili wako?
-
• Ni sifa gani ya kiroho utachagua kuendeleza ?
Roho wa Binadamu
Roho yako ni chombo cha milele. Bwana alimwambia nabii wake Ibrahimu: “Wewe ulichaguliwa kabla hujazaliwa.”15 Bwana alisema kitu sawa kuhusu Yeremia16 na wengine wengi.17 Aliisema hata kukuhusu wewe.18
Baba yako wa Mbinguni amekufahamu kwa muda mrefu sana. Wewe, kama mwanawe au bintiye, aliyechaguliwa naye ili kuja duniani kwa wakati huu sahihi, ili kuwa kiongozi katika kazi Yake kubwa duniani.19 Ulichaguliwa sikwa ajili ya tabia yako ya kimwili lakini kwa ajili ya sifa zako za kiroho kama vile uhodari, ujasiri, uadilifu wa moyo, kiu ya kweli, njaa kwa ajili ya hekima, na hamu ya kuwatumikia wengine.
Ulikuzaa baadhi ya sifa hizi kabla ya kuzaliwa. Zingine unaweza kuendeleza hapa duniani20 unapozitafuta kwa dhati.21
Sifa muhimu ya kiroho ni ile ya umahiri wa kibinafsi---uwezo wa kuweka sababu mbele ya tamaa. Umahiri wa kibinafsi hujenga dhamiri imara. Na dhamiri yako huamua majibu yako ya kimaadili katika hali ngumu, ya majaribu, na yenye changamoto. Kufunga husaidia roho yako kuendeleza utawala juu ya tamaa yako ya kimwili. Kufunga pia huongeza upatikanaji wako wa msaada wa mbinguni, kunapoongeza maombi yako. Kwa nini kuwe na haja ya umahiri wa kibinafsi? Mungu aliweka tamaa kali ndani yetu kwa chakula na upendo, muhimu ili familia ya binadamu iendelee kudumu.22 Tunapotawala tamaa zetu ndani ya mipaka ya sheria za Mungu, tunaweza kufurahia maisha marefu, upendo mkuu, na shangwe kamili.23
Haishangazi basi, kwamba majaribu mengi ya kupotea kutoka kwa mpango wa Mungu wa furaha huja kwa njia ya matumizi mabaya ya tamaa hizo muhimu, zilizotolewa na Mungu. Kudhibiti tamaa zetu daima si rahisi. Hakuna mmoja wetu anayezidhibiti kikamilifu.24 Makosa hutokea. Makosa hufanywa. Dhambi hutendwa. Tufanye nini basi? Tunaweza kujifunza kutoka kwazo. Na tunaweza kutubu kikweli.25
Tunaweza kubadili tabia zetu. Tamaa zetu zinaweza kubadilika. Vipi? Kuna njia moja tu. Mabadiliko ya kweli—mabadiliko ya kudumu—yanaweza kuja tu kwa njia ya uponyaji, utakaso, na nguvu ya kuwezesha ya Upatanisho wa Yesu Kristo.26 Anakupenda—kila mmoja wenu!27Anakuruhusu kutapata uwezo Wake unaposhika amri Zake, kwa hamu, na kwa bidii. Ni rahisi hivyo na hakika. Injili ya Yesu Kristo ni injili ya mabadiliko!28
Nafsi ya binadamu yenye nguvu, yenye udhibiti juu ya tamaa ya mwili, ni mtawala juu ya hisia na tamaa na si mtumwa kwao. Aina hiyo ya uhuru ni muhimu kwa roho kama oksijeni ilivyo kwa mwili! Uhuru kutoka kwa utumwa wa kibinafsi---ni ukombozi wa kweli!29
Tuko “huru kuchagua uhuru na uzima wa milele ... au kuchagua utumwa na kifo.”30Tunapochagua njia ya juu inayoelekea kwa uhuru na uzima wa milele, njia hiyo hujumuisha ndoa.31 Watakatifu wa Siku za Mwisho wanatangaza kwamba “ndoa kati ya mwanaume na mwanamke imeteuliwa na Mungu na kuwa familia ni muhimu kwa mpango wa Muumba kwa hatima ya milele ya watoto wake.” Tunajua pia kwamba “jinsia ni sifa muhimu ya maisha ya mtu kabla ya kuzaliwa, maisha ya duniani, na utambulisho wa milele na kusudi.”32
Ndoa kati ya mwanaume na mwanamke ni ya msingi katika mafundisho ya Bwana na muhimu kwa mpango wa Mungu wa milele. Ndoa kati ya mwanaume na mwanamke ni mfano wa Mungu kwa ukamilifu wa maisha duniani na mbinguni. Mfumo wa Mungu wa ndoa hauwezi kudhulumiwa, kueleweka vibaya, au kufasiriwa vibaya.33 Si kama unataka furaha ya kweli. Muundo wa Mungu wa ndoa unalinda uwezo mtakatifu wa uzazi na shagwe ya urafiki wa kweli wa ndoa.34 Tunajua kwamba Adamu na Hawa walioozwa na Mungu kabla ya kuona furaha ya kuungana kama mume na mke.35
Katika siku zetu, serikali za kiraia zina upendeleo fulani katika kulinda ndoa kwa sababu familia zenye nguvu zinajumuisha njia bora ya kutoa afya, elimu, ustawi, na ustawi wa vizazi vinavyoinuka.36 Lakini serikali za kiraia zinasukumwa sana na mwenendo wa kijamii na falsafa za kidunia wanapoandika, kuandika upya, na kutekeleza sheria. Bila kujali aina ya sheria za kiraia zinazoweza kutungwa, mafundisho ya Bwana kuhusu ndoa na maadili hayawezi kubadilishwa.37 Kumbuka: dhambi, hata ikihalalishwa na mwanadamu, bado ni dhambi machoni pa Mungu!
Wakati tunapohitajika kuiga wema na huruma ya Mwokozi wetu, wakati tunapohitajika kuthamini haki na hisia za watoto wote wa Mungu, hatuwezi kubadilisha mafundisho Yake. Si nafasi yetu kubadilisha. Mafundisho yake ni yetu kujifunza, kuelewa, na kuzingatia .
Njia ya maisha ya Mwokozi ni nzuri. Njia yake inajumuisha usafi wa kimwili kabla ya ndoa na uaminifu kamili ndani ya ndoa.38 Njia ya Bwana ndiyo njia pekee kwetu ya kupata furaha ya kudumu. Njia yake huleta faraja endelevu kwa roho zetu na amani ya kudumu kwenye nyumba zetu. Na bora kuliko yote, njia yake inatuelekeza nyumbani Kwake na kwa Baba yetu wa Mbinguni, kwa uzima wa milele na kuinuliwa.39 Huu ndiyo msingi muhimu wa kazi na utukufu wa Mungu.40
Ndugu na dada zangu wapwendwa, kila siku ni siku ya uamuzi, na maamuzi yetu huamua hatima yetu. Siku moja kila mmoja wetu atasimama mbele ya Bwana katika hukumu.41 Kila mmoja wetu atakuwa na mahojiano binafsi na Yesu Kristo.42 Tutawajibika kwa maamuzi tuliyofanya kuhusu miili yetu, sifa zetu za kiroho, na jinsi tulivyoheshimu muundo wa Mungu wa ndoa na familia. Ili tuweze kuchagua kwa hekima maamuzi ya kila siku kwa milele ndilo ombi langu la dhati katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.