2010–2019
Tazama Mbele na Uamini
Oktoba 2013


10:32

Tazama Mbele na Uamini

Katika macho ya Bwana, si sana sana kile tumefanya au pale tumefika bali ni pale sisi tuko tayari kwenda.

Nilipokuwa kijana, nikiwa nafanya kazi katika mashamba pamoja na mama yangu, alinifundisha mojawapo wa masomo muhimu katika maisha. Muda ulikuwa umeenda asubuhi, jua lilikuwa limechomoza na tulikuwa tunalima kwa kile nilichokifiria kuwa ni muda mrefu sana. Nilisimama na kuangalia nyuma kwa kile ambacho tulikuwa tumekitimiza na kumwambia mama yangu, “Tazama kile tulichokifanya!” Mama hakujibu. Nikifikiria kwamba hakunisikia, nilirudia kile nilichokisema kwa sauti ya juu. Bado hakujibu. Nikisema kwa sauti ya juu zaidi, nilirudia tena. Mwishowe, alinigeukia na kusema, “Edward, usiangalie nyuma kamwe, tazama mbele kwa kile ambacho bado ni lazima tukifanye.”

Ndugu na dada zangu wapendwa, maagano tuliyoyafanya na Bwana tulipobatizwa, “kusimama kama mashahidi wa Mungu wakati wote na katika kila kitu, na katika sehemu zote ambazo tutakuwa” (Mosia 18:9), ni ahadi ya maisha yetu yote. Rais Dieter F. Uchtdorf ameshauri: “Wale walioingia katika maji ya ubatizo na kupokea karama ya Roho Mtakatifu na wameweka miguu yao katika njia ya ufuasi na wamepewa jukumu la kumfuata kiadilifu na kiuaminifu katika njia za Mwokozi wetu” (“Saints for All Seasons,” Ensign au Liahona, Sept. 2013, 5). Bwana, kwa kupitia kwa watumishi Wake hutuita kuhudumu katika wito tofauti, ambazo tunazikubali kwa ahadi kamili. Pale kuachiliwa kunapofanywa na wito katika kazi tofauti kutolewa, kwa furaha tunakubali tukijua, kama wenzetu walioenda mbele yetu walivyojua, kwamba, “katika huduma ya Bwana, si wapi unatumikia ila ni kwa jinsi gani” (J. Reuben Clark Jr., in Conference Report, Apr. 1951, 154).

Hivyo wakati Rais wa Kigingi au Askofu anapoachiliwa, kwa furaha anakubali kuachiliwa huko, na wakati wito unapotolewa kutumikia katika namna nyingine ambayo Bwana, kwa kupitia watumishi Wake, “anaona inafaa” (Mosia 3:19), hafunikwi na wingu la uzoefu uliopita, au haangalii nyuma na kufikiria kwamba ametumikia vya kutosha. Yeye “Hachoki katika kufanya mema,” kwa sababu anajua kwamba “anaweka msingi wa kazi kubwa” akiwa na ono dhabiti kwamba juhudi hizo hubariki maisha kwa milele. Hivyo “kutokana na mambo madogo huja yale yaliyo makuu”(M&M 64:33).

Sisi sote inatupasa “kujishughulisha kwa shauku katika kazi njema, na kufanya mambo mengi kwa hiari yao wenyewe, na kutekeleza haki nyingi” (M&M 58:27).

Mzee Jeffrey  R. Holland wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alishauri: “Yakale yatufundishe na siyo ya kuyaishi. Tunatazama nyuma kudai makaa kutoka kwenye uzoefu unaowaka na si majivu. Na tunavyokuwa tumejifunza kile tunachokihitaji na tumepata ubora ambao tumepata uzoefu wake, hivyo tunatazama mbele na kukumbuka kwamba imani mara zote imeelekeza kwa siku za usoni” (“The Best Is Yet to Be,” Ensign, Jan. 2010, 24; au Liahona, Jan. 2010, 18).

Hali somo la mama yangu la kutazama mbele lilikuwa limeelekezwa katika magugu yanayoonekana katika shamba, changamoto hiyo ilikuwa ndogo kulinganisha na kile ambacho watakatifu wa kale walipitia. Mzee Joseph  B Wirthlin aliezea tukio hili vyema sana: “Mnamo mwaka 1846, zaidi ya watu 10,000 waliondoka mji uliokuwa na ustawi wa Nauvoo ambao ulikuwa umejengwa pembezoni mwa Mto Mississippi. Wakiwa na imani katika viongozi wao wa kinabii, washiriki hao wa kale wa kanisa waliacha ‘Urembo wa Mji’ wa mji wao na wakakimbilia nyikani mwa mipaka ya Amerika. Hawakujua haswa kuwa walikuwa wanaenda wapi, kiuhakika kulikuwa na maili ngapi mbele yao, na kwa mda gani safari ingechukua, au ni vipi maisha yao ya mbele yangekuwa. Lakini wao walijua walikuwa wanaongozwa na Bwana na watumishi Wake” (“Faith of Our Fathers,” Ensign, Mei 1996, 33).

Walijua ilikuwa vipi kutazama mbele na kuamini. Katika kipindi cha miaka kumi na nusu baadaye, baadhi ya washiriki hawa walikuwepo wakati ushuhuda ulipopokelewa:

“Kwani amini ninawaambia, heri yule ashikaye amri zangu, iwe katika maisha au kifo; na yule aliye mwaminifu katika taabu, thawabu yake ni kubwa katika ufalme wa mbinguni.

“Hamuwezi kuona kwa macho yenu ya asili, kwa wakati huu, mipango ya Mungu wenu juu ya mambo yale ambayo yatakuja hapo baadaye, na utukufu utakaofuata baada ya taabu kubwa” (M&M 58:2–3).

Sisi pia tunaweza kutazama mbele na kuamini. Tunaweza kukumbatia mwaliko wa Bwana wetu, ambaye kwa mikono iliyonyooka anatualika:

“Njooni kwangu, ninyi wote mnaolemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

“Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu.

“Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”(Mathayo 11:28–30).

Nabii wetu mpendwa, Rais Thomas S. Monson; washauri wake; na Jamii ya Mitume kumi na wawili wametoa mwaliko kwetu sisi kushiriki katika kazi ya wokovu. Waongofu wapya, vijana, na vijana wazima, wale ambao wamestaafu katika kazi zao za ujuzi, na wamisionari wanahitaji kufanya kazi pamoja katika kuharakisha kazi ya wokovu.

Rais Boyd  K. Packer, Rais wa Jamii ya Mitume kumi na wawili alihudhuria shindano la kuvuta la ng’ombe dume, ambapo alipata mfano. Aliezea ujuzi huu: “Sleji ya mbao ilikuwa imewekwa matofali ya simenti: ratili elfu kumi [kilo 4,535 ]---tani tano … Lengo lilikuwa ni dume wavute slegi futi tatu [sentimeta 91 cm]. … Niligundua jozi lililowiana la wanyama wakubwa sana, waliotiwa nira wa mchanganyiko wa rangi ya bluu-kijivu …dume wakubwa wa rangi blue wa kipindi kilichopita.”

Katika kuzungumzia matokeo ya shindano lililopita, alisema: “Timu zilishindwa moja baada ya ingine…..Dume wa bluu hawakufua dafu! Wanyama wawili wadogo wasiotambulika, na hawakuwiana vyema, walivuta slegi mara zote tatu.”

Halafu tena alipewa maelezo katika matokeo ya kushangaza: “Wale wakubwa wawili wa blue walikuwa na nguvu zaidi na walifanana kwa ukubwa zaidi ya timu nyingine. Lakini dume wadogo walifanya kazi kwa pamoja na kwa kushirikiana. Walilivuta kongwa kwa pamoja. Wanyama wote walilinyanyua mbele katika wakati ule ule na wakalazimisha mzigo kuenda” (“Equally Yoked Together,” address delivered at regional representatives’ seminar, Apr. 3, 1975; in Teaching Seminary: Preservice Readings [2004], 30).

Tunapotazama mbele na kuamini, tunahitaji ushirikiano kama huu katika kuharakisha kazi ya wokovu tunapowaalika wengine kuja kwa Kristo. Katika uwezo wetu tofauti, tunahitaji kufuata ushauri wa Rais Dieter  F. Uchtdorf “kusimama karibu pamoja na kuinua pale tunaposimama” Ensign or Liahona, Nov. 2008, 56). Tunaweza kufikia uwezo wetu, kama ilivyotambulika na Mzee L. Tom Perry wa Jamii ya Mitume kumi na wawili: “Ninavyosafiri sehemu nyingi za Kanisa ninashangazwa na mambo mengi chanya yanayotokea. Na hivyo sijawahi kuhisi kwamba, sisi kama watu, tunaishi katika uwezo wetu kamili. Fikra zangu ni kwamba si mara zote tunafanya kazi kwa kushirikiana, kwamba bado tunafurahia katika mataminio ya heshima zetu binafsi na mafanikio, na tunaonesha hamu kidogo tu katika malengo ya pamoja ya kuujenga ufalme wa Mungu” (“United in Building the Kingdom of God,” Ensign, May 1987, 35).

Na tuungane katika lengo moja “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39).

Mwokozi wetu, Yesu Kristo, ambaye huona kutoka mwanzo mpaka mwisho, alijua vyema njia ambayo angeitumia kusafiria kwenda Gethsemane na Golgotha aliposema, : “Mtu ye yote ashikaye jembe kuanza kulima kisha akawa anageuka kutazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.” (Luka 9:62).Katika macho za Bwana, si sana sana kile tumefanya au pale tumefika bali ni pale sisi tuko tayari kwenda.

Kanuni zetu zinazotuongoza zilifundishwa kwetu na Nabii Joseph Smith: “Kanuni za msingi za dini yetu ni shuhuda za Mitume na Manabii, kuhusu Yesu Kristo, kwamba alikufa, alizikwa, na alifufuka tena siku ya tatu, na akapaa mbinguni; na mambo mengine ambayo yanahusu dini yetu ni viambatisho vya hayo” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 49).

Ninashuhudia kwamba tunavyofuata mfano wa Mwokozi wetu, Yesu Kristo, na kuinua mikono yetu katika mraba katika tendo la kumkubali nabii wetu Mpendwa, Rais Thomas  S. Monson, tunapata amani, faraja, na furaha na “watakula mema ya Sayuni …. katika siku za mwisho.(M&M64:34). Katika Jina la Yesu Kristo, amina.