2010–2019
Sisi Tuna Sababu Kuu ya Kufurahia
Oktoba 2013


12:48

Tuna Sababu Kubwa ya Kufurahia

Wakati ninyi mnapopenda, mnapotunza, na kuwahudumia wengine katika njia ndogo na rahisi, mnakuwa watendaji hai katika kazi ya wokovu.

Wakati baba mkwe wangu alianga dunia, familia yangu ilikusanyika pamoja kuwasalimu wengine ambao walikuja na kutoa heshima zao. Jioni yote nilipokuwa nikiongea na familia na marafiki, kila mara niliona mjukuu wangu wa miaka 10, Porter, akisimama karibu na mama mkwe---“bibi” yake. Wakati mwengine alikuwa anasimama nyuma yake, alimtazama. Mara moja niliona ameunganisha mkono wake naye. Nilimwona akishikilia mikono yake polepole, na kumpatia kumbatio dogo, na kusimama kando yake.

Siku kadhaa baada ya tukio hili, singeweza kuondoa picha hii katika akili yangu. Nilipata kumtumia Porter barua, nikimwambia kile nilikuwa nimeona. Nilimtumia barua pepe na kumwambia kile nilikuwa nimeona na kuhisi. Nilimkumbusha Porter kuhusu maagano yeye alikuwa amefanya wakati alibatizwa, nikinukuu maneno ya Alma katika Mosia mlango wa 18::

“Na ikawa kwamba aliwaambia: Tazameni, hapa kuna maji ya Mormoni (kwani hivi ndivyo yaliitwa) na sasa, kwa vile mnatamani kujiunga na zizi la Mungu, na kuitwa watu wake, na mko radhi kubeba mizigo ya mmoja na ya mwingine, ili iwe mepesi;

“Ndio, na mko tayari kuomboleza na wale wanaoomboleza; ndio, na kufariji wale ambao wanahitaji kufarijiwa, na kusimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote na katika vitu vyote, na katika mahali popote mlipo, hata hadi kifo, … ili muweze kukombolewa na Mungu, na kuhesabiwa pamoja na wale wa ufufuko wa kwanza, ili mpokee uzima wa milele—

“ … Ikiwa hili ndilo pendo la mioyo yenu, ni nini mnacho dhidi ya kubatizwa kwa jina la Bwana, kama ushahidi mbele yake kwamba mmeingia kwenye agano na yeye, kwamba mtamtumikia na kushika amri zake, ili awateremshie Roho yake juu yenu zaidi?”1

Mimi nilimwelezea Porter kwamba Alma alifunza kwamba wale ambao wanataka kubatizwa wanahitaji kuwa radhi kumtumikia Bwana kwa kuwatumikia wengine---kwa maisha yako yote! Mimi nilisema: “Sijui kama ulielewa, lakini vile ulimwonyesha upendo na kumjali Bibi, ilikuwa inapelekana na maagano yako. Tunaweka maagano yetu kila siku tunapokuwa wakarimu, tunapoonyesha upendo, na kutunzana. Nilikuwa nataka ujue mimi najivunia juu yako kwa kuwa mweka maagano! Kadiri unavyoweka maangano uliyofanya wakati ulibatizwa, utakuwa tayari kutawazwa katika ukuhani. Hii agano la ziada litakupatia nafasi zaidi za kubariki na kuwahudumia wengine na kukusaidia kujitayarisha kwa maagano ambayo utafanya katika mahekalu. Asante sana kwa kuwa mfano mzuri jinsi hiyo kwangu! Asante kwa kunionyesha vile inaonekana kuwa mweka maagano!”

Porter alijibu tena: “Bibi, asante kwa ujumbe huu.Wakati wote nilipokuwa nikimkumbatia Bibi, sikujua kwamba nilikuwa ninaweka maagano yangu, lakini nilihisi vuguvugu katika moyo wangu na nikahisi vyema zaidi. Najua kwamba ilikuwa ni Roho Mtakatifu katika moyo wangu.”

Mimi pia nilihisi vuguvugu katika moyo wangu nilipogundua kwamba Porter ameelewa kuweka maagano yake na ahadi ya “daima kuwa na Roho Yake kuwa [nasi]”2—ahadi iliyowezeshwa na kupokea karama ya Roho Mtakatifu.

Kina dada, ninapowatembelea ulimwenguni kote, nimeona kwamba wengi wenu mko kama Porter. Kwa utulivu mnasimama kama mashahidi wa Mungu, mnaomboleza na wale wanaoomboleza, mnafariji wale wanaohitaji faraja bila kufahamu kwamba mnaweka maagano yenu mliofanya katika maji ya ubatizo na katika hekalu. Mnapoonyesha upendo, mnapotunza, na mnapowahudumia wengine katika njia ndogo na rahisi, mu washiriki hai katika kazi ya wokovu, kazi ya Mungu ya “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu.”3

Kama “mabinti katika ufalme wa [Bwana],”4 tumefanya maagano matakatifu. Tunatembea katika kile Nefi alikiita “njia nyembamba iliyosonga ambayo inaelekea uzima wa milele.”5 Sisi sote tuko katika sehemu tofauti katika njia. Lakini tunaweza kufanya kazi pamoja ili kusaidiana “msonge mbele mkiwa na imani imara katika Kristo, mkiwa na mng’aro mkamilifu wa tumaini, na upendo kwa Mungu na wanadamu wote.”6

Jeane anahudumu kama mshauri wa Wasichana. Miezi kadhaa iliyopita alijua kuhusu shughuli iliyokuwa inatarajiwa ya vijana katika kata: kupanda sehemu inayoitwa Kilele cha Malan. Yeye alisisimuka kwa sababu alikuwa majuzi ameweka lengo la kukwea huko.

Alipowasili katika mwanzo wa njia, Ashley, rafiki yake wa dhati alimjia. Akiunganisha mikono na Jeane, alijitolea kutembea pamoja naye, akisema, “Mimi nitaenda pamoja nawe.” Ashley ambaye alikuwa umri wa miaka 16 wakati huo, alikuwa na changamoto za kimwili ambazo zilimfanya yeye kuwa na shida ya kukwea haraka haraka. Kwa hivyo yeye na Jeane walitembea pole pole, wakitazama uumbaji wa Baba ya Mbinguni: miamba kwenye kilele cha mlima juu yao, na maua yaliyowazunguka. Jeane baadaye alisema, “Hakika haukinichukua mimi muda mrefu kusahau kuhusu lengo langu la kutembea hadi kwenye kilele, kwani punde kwa sababu ya tukio la ajabu la aina ingine ---tukio la ajabu la kutaja urembo iliyopo njiani, ambao wingi wake, mimi nisingeuona kama mimi ningetembea tu kufikia lengo la kilele cha Malan.”

Vile Jeane na Ashley waliendelea kutembea, huko nyuma kabisa ya kundi, Emma alijiunga nao, msichana mwengine katika kata, ambaye aliamua kuwangojea na kutembea pamoja nao. Emma aliongeza furaha yao. Aliwafunza wimbo na kutoa uhimili na kuwatumainisha. Jeane anakumbuka: “Sisi tulikaa chini na tukapumzika, sisi tuliimba, tukaongea, na tukacheka. Mimi niliweza kuwajua Ashley na Emma katika njia ambayo singeweza kivingine. Haikuwa ni kuhusu mlima usiku huo---ilikuwa zaidi sana, sana kabisa. Ilikuwa ni kuhusu kusaidiana mmoja na mwengine huko njiani, hatua moja kwa wakati mmoja.

Jeane, Ashley, na Emma walipokuwa wakitembea waliimba na wakapumzika na wakacheka pamoja, wao labda hawakuwa wakifikiria, “Lo! sisi tunaweka maagano yetu sasa.” Lakini walikuwa wanaweka maagano yao. Walikuwa wanahudumiana kwa upendo, ufadhili, na azimio. Walikuwa wanaimarishana imani walipokuwa wanatiana moyo, na kuhudumiana mmoja na mwengine.

Mzee Russell  M. Nelson alifunza: “Wakati tanagundua kwamba sisi ni watoto wa agano, tunajua sisi ni kina nani na kile Mungu anatarajia kutoka kwetu. Sheria Yake inaandikwa katika mioyo yetu.”7

Maria Kuzina ni binti wa agano wa Mungu ambaye anajua yeye ni nani na kile Mungu anatarajia kutoka kwake. Wakati alinikaribisha nyumbani kwake katika Omsk, Russia, nilifikiria nilikuwa hapo kumuhudumia, lakini punde niligundua kuwa mimi nilikuwa hapo kujifunza kutoka kwake. Mwongofu katika Kanisa, Maria huishi kwa maelekezo yanayopatikana katika Luka 22: “Utakapoongoka waimarishe ndugu zako.”8 Yeye ana imani katika maneno ya nabii wetu aliye hai, Rais Thomas  S. Monson, ambaye alisema:

“Sasa ndiyo wakati wa washiriki na wamisionari kuja pamoja, kufanya kazi pamoja, kutumika katika shamba ya mzeituni la Bwana kuleta nafsi Kwake. …

“Tunapotenda katika imani Bwana atatuonyesha jinsi ya kuimarisha Kanisa Lake katika kata na matawi ambapo tunaishi. Yeye atakuwa pamoja nasi na atakuwa mwenzi hai katika kazi zetu za umisionari.

“ … Mfanye imani yenu … mnapofikiria kwa maombi ni kina nani kati ya familia zetu, marafiki zetu, majirani wetu, na watu mnaofahamiana nao ambao mngependa kuwaalika kuja katika nyumba yenu kukutana na wamisionari, ili kwamba waweze kusikia ujumbe wa Urejesho.”9

Maria hufuata ushauri huu kwa kuwatunza na kuwahudumia kina dada ambao ameombwa kuwatembelea na pia kwenda zaidi ya kazi. Yeye ana marafiki wengi ambao si wahudhuriaji kamili au wengine ambao bado hawajasikia ujumbe wa injili ya urejesho ya Yesu Kristo. Kila siku yeye hufanya imani na kuomba ili ajue ni nani anayehitaji usaidizi wake, na kisha yeye hutenda kulingana msukumo anaopokea. Yeye hupiga simu, kuonyesha upendo wake, na kuwaambia marafiki zake, “Tunakuhitaji.” Yeye anakuwa na jioni ya familia nyumbani katika nyumba yake kila wiki na hualika majirani, washiriki, na wamisionari kuja---na yeye huwalisha. Yeye huwaalika wao kuja kanisani, huwatunza. Na hukaa karibu na wao wanapokuja.

Maria anaelewa ukumbusho wa majuzi wa Mzee Jeffrey  R. Holland kwamba “mwaliko ambao huzaliwa na upendo wetu kwa wengine na kwa Bwana Yesu Kristo … kamwe hautaonekana kama chukizo au kitu cha kuhukumu.”10 Yeye huweka orodha ya watu ambao wanasema kuwa wamechukizwa, naye huendelea kuwahudumia. Kwa sababu wanajua kwamba anawapenda, anaweza kuwaambia, “Msichukizwe. Huu ni mzaha!”

Maria ni mfuasi---mweka agano wa Yesu Kristo. Ingawa hana mwenye ukuhani katika nyumba yake, yeye huhisi nguvu za Mungu kila siku katika utimizo wa maagano yake ya hekalu kadiri anavyosonga mbele kwenye njia, kuendelea hadi mwisho na akiwasaidia wengine kushiriki katika kazi ya wokovu njiani.

Nilipokuwa ninashiriki uzoefu huu, Je! Wewe ulijiona ukiwa katika kazi ya wokovu? Chukua muda mchache wa kufikiria kuhusu dada mwengine wa Mungu ambaye anahitaji kutiwa moyo ili arudi katika njia ya agano, au ambaye anahitaji usaidizi kidogo ili kukaa katika njia. Muulize Baba yako wa Mbinguni kumhusu. Yeye ni binti Yake. Anamjua kwa jina. Anakujua wewe, na atakuambia kile anachohitaji. Kuwa na subira na uendelee katika imani na maombi kwa niaba yake, na utende juu ya misukumo unayopokea. Unapotenda juu ya misukumo hii, Roho atadhibitisha kwamba toleo lako linakubalika Kwake Bwana.

Dada Eliza R. Snow … alikiri kwa shukrani juhidi za akina dada za kuimarishana. Aliwaambia kwamba ingawa Kanisa halikuweka kumbukumbu ya kila mchango walitoa ili kuwasaidia wenye mahitaji, Bwana aliweka kumbukumbu kamili ya kazi yao ya kuokoa:

“‘ … Rais Joseph Smith alisema muungano huu uliundwa ili kuokoa nafsi. Je, tunafanya nini ili kuwarudisha wale waliopotoka?--- Kutia joto mioyo ya wale waliokuwa baridi katika injili?--- Kitabu kingine kinawekwa kwa ajili ya imani yenu, ukarimu wenu, vitendo vyenu vyema, na maneno [yako]. Kumbukumbu ingine inawekwa. Hakuna chochote kinachopotea.’”11

Katika Kitabu cha Mormoni, Amoni huongea juu ya sababu kuu zetu kufurahia. Yeye husema: “Na sasa, nauliza, ni baraka gani kubwa ambayo [Mungu] ametupatia sisi? Mnaweza kunena?

Katika msisimko wake, Amoni hakawii kujibu. Yeye anasema,“Tazama, ninajibu kwa niaba yenu; … hii ndiyo baraka ambayo tumeteremshiwa, kwamba tumetengenezwa kuwa vyombo mikononi mwa Mungu kuimarisha kazi hii kubwa.”12

Sisi ni mabinti wa agano katika ufalme wa Bwana, na tuna nafasi ya kuwa vyombo katika mikono Yake. Tunaposhiriki katika kazi ya wokovu kila siku katika njia ndogo na rahisi---tukitunzana, kuimarishana, na kufunzana mmoja na mwengine---tunaweza kujiunga pamoja na Amoni, ambaye alitamka:

“Lakini tazama, shangwe yangu ni tele, ndio, moyo wangu umejawa na shangwe, na nitafurahi ndani ya Mungu wangu.

“Ndio, najua kwamba mimi si kitu; kulingana na nguvu zangu mimi ni mlegevu; kwa hivyo sitaweza kujivuna mwenyewe, lakini nitajivuna katika Mungu wangu, kwani kwa nguvu zake ninaweza kufanya vitu vyote.”13

Juu ya haya mimi nashuhudia, katika jina la Yesu Kristo, amina.