2010–2019
Kukabiliana na Changamoto za Ulimwengu wa Leo
Oktoba 2015


14:33

Kukabiliana na Changamoto za Ulimwengu wa Leo

Chaguo tunazofanya—misheni, elimu, ndoa, ajira, na huduma katika Kanisa—zitajenga hatima yetu ya milele.

Mengi yameandikwa na kusemwa kuhusu kizazi cha leo cha vijana wazima. Utafiti unaonyesha kwamba wengi wanapinga dini yenye utaratibu. Wengi wana madeni na hawana ajira. Wengi wao wanapenda wazo la ndoa, lakini wengi wanaogopa kuchukua hatua hiyo. Idadi inayoongezeka haitaki watoto. Bila injili na mwongozo wenye maongozi, Wengi wanazunguka-zunguka katika njia ngeni na wanapoteza njia zao.

Kwa bahati nzuri, vijana wazima waumini wa Kanisa wamebakia nyuma katika mielekeo hii inayosumbua, kwa kiasi, kwa sababu tumebarikiwa na mpango wa injili. Mpango ule unajumuisha kushikilia kwa nguvu fimbo ya chuma—kujishikilia kwenye neno la Mungu na neno la manabii Wake. Tutashikilia fimbo ambayo inatuelekeza kurudi kwake? Sasa ni “siku ya kuchagua”1 kwetu sote.

Nilipokuwa mvulana, wakati nilipokuwa karibu kufanya uchaguzi ambao nilikuwa sijaukagua vyema, baba yangu wakati mwingine angesema, “Robert, kuwa makini na ufanye kile unachojua ni sahihi! Ninyi mmeshapitia hayo. Katika roho ya mazungumzo yake ya wazi, ningependa kusema hususani kwenu vijana—vijana waungwana—vijana wazima wetu waungwana, kwani “roho yangu hufurahia katika uwazi ... ili kwamba [tuweze] kujifunza.”2

Mnaishi katika kipindi cha muda muhimu cha maisha yenu. Chaguzi mnazofanya—misheni, elimu, ndoa, ajira na huduma katika Kanisa—zitawaletea uzoefu milele. Hii inamaanisha siku zote lazima muwe mnalenga mbele—mkilenga siku zijazo.

Kama rubani katika Jeshi la Anga, nilijifundisha kanuni hii: kamwe usiruke kwa makusudi katika mvua ya radi. (Mimi sitakwambia jinsi nilivyogudua hayo.) Badala yake izunguke, chukua njia ingine, au ngoja dhoruba iishe kabla ya kutua.

Wapendwa vijana wazima, ndugu na akina dada, Nataka kuwasaidia “kuruka kwa usahihi” wakati wa dhoruba za siku za mwisho zinapotanda. Ninyi ni marubani. Wajibu wenu ni kufikiri kuhusu matokeo ya kila uchaguzi. Jiulizeni wenyewe, ”Kama nikifanya uchaguzi huu, ni kitu ngani kibaya sana ambacho kinaweza kutokea?” Uchaguzi wenu sahihi utawasaidia msichepuke kutoka kwenye mwelekeo sahihi.

Fikirieni kuhusu hilo: Kama mtachagua kutokunywa pombe, hamtakuwa mlevi! Kama kamwe hamtachagua kuwa na madeni, mtaepuka uwezekano wa kufilisika!

Mojawapo ya madhumumi ya maandiko ni kutuonyesha jinsi watu wenye haki wanajibu majaribu na uovu. Kwa kifupi, Yaepuke! Yusufu alimkimbia mke wa Potifa.3 Lehi alichukuwa familia yake na waliondoka Yerusalemu.4 Mariamu na Yusufu walikimbilia Misri kutoroka njama ovu ya Herode.5 Katika kila mfano, Baba wa Mbinguni aliwatahadharisha waumini hawa. Vilevile, Yeye atatusaidia sisi kujua kama tupigane, tukimbie, au kukubali hali zetu zinazobadilika. Yeye atanena kwetu kupitia sala, wakati tunaposali, tutakuwa na Roho Mtakatifu, ambaye atatuongoza. Tuna maandiko, mafundisho ya manabii wanaoishi, baraka za Baba mkuu, ushauri wa kutia moyo wa wazazi na viongozi wa ukuhani na makundi saidizi, na zaidi ya hao, sauti ndogo tulivu ya Roho.

Bwana daima ataweka ahadi Yake: “Nitakuongoza siku zote.”6 Swali pekee ni, tutajiachia wenyewe tuongozwe? Tutasikia sauti Yake na sauti za watumishi Wake?

Ninashuhudia kwamba kama upo hapo kwa ajili ya Bwana, Yeye atakuwepo kwa ajili yako.7 Kama unampenda Yeye na kutii amri Zake, utakuwa na Roho Wake apate kuwa pamoja nawe na kukuongoza. “Weka imani yako katika Roho yule ambaye anakuongoza kufanya mema. ... Kwa hii tutajua vitu vyote ... kuhusu vitu vya haki.”8

Pamoja na kanuni hizo kama msingi, naweza kuwapeni ushauri kiasi wa kiutendaji?

Wengi wa kizazi chenu wanakabiliwa na madeni makubwa mno. Wakati nilipokuwa kijana, Rais wa kigingi changu alikuwa Mkurugenzi wa banki ya kitega uchumi kwenye Wall Street. Alinifundisha, “Wewe ni tajiri kama unaweza kuishi kwa furaha kwa njia ambayo unatumia kidogo kuliko kipato chako. Unaweza kufanya vipi? Lipa zaka yako na kisha weka akiba! Wakati unachuma zaidi, weka akiba zaidi. Usishindane na wengine kuwa na vitu vya gharama. Usinunue kile usichoweza kukimudu.

Vijana wengi katika ulimwengu wanaingia kwenye madeni kupata elimu na baadaye wanakuta gharama ya shule ni kubwa mno kuliko wanavyoweza kulipa. Tafuta msaada wa masomo, mikopo isiyo na riba. Pata ajira ya muda, na kama inawezekana, ikusaidie kulipa gharama yako mwenyewe. Hii itahitaji dhabihu kiasi, lakini itawasaidia kufanikiwa.

Elimu hukutayarisha kwa nafasi nzuri za ajira. Huwaweka kwenye nafasi nzuri ya kuhudumu na kuwabariki wale walio karibu nanyi. Itawaweka kwenye njia kujifunza ya maisha yote. Itawaimarisha kupigana dhidi ya upumbavu na makosa. Kama vile Joseph Smith alivyofunza: “Elimu huondosha giza, wasi wasi na shaka; kwa haya hayawezi kuwepo pale elimu ilipo. ... Katika elimu kuna uwezo.”9 “Lakini kuelimika ni vyema ikiwa watatii mawaidha ya Mungu.”10 Elimu itawatayarisha ninyi kwa kile kilicho mbele, ikijumuisha ndoa.

Tena, naomba niseme wazi kabisa? Njia ile inayoelekea kwenye ndoa hupitia upeo unaoitwa miadi! Miadi ni nafasi ya mazungumzo marefu. Wakati mnafanya miadi, jifunze kila kitu kuhusu nyote wenyewe. Jifahamisheni na familia inapowezekana. Je! Malengo yenu yanambatana? Je! Mnashiriki hisia sawa kuhusu maandiko, Mwokozi, ukuhani, hekalu, ulezi, wito wa Kanisani, na kuwahudumia wengine? Je! Mshaangliana kwa makini mnapokabiliwa shida, mjibizo wa fanaka, ushinde, kujizuia ghadhabu, na kukabilia na vikwazo? Je! Yule anayefanya miadi naye uvuruga watu ama huwajenga? Je! Mtazamo na lugha na mwenendo wake ndiyo vile ungependa kuishi navyo kila siku?

Baada ya hayo yote, hakuna kati yetu anayeowa mtu aliye kamili; tunaoa mwenye uwezo. Ndoa sahihi si tu ile inayohusu nini tunataka; ni kuhusu nini anachotaka na kile—yule ambaye atakuwa mwenzi wangu—anataka na anahitaji mimi niwe.

Tukisema kwa uwazi, tafadhali usiwe na miadi katika umri wako wote wa miaka ya 20 ili tu “ujifurahishe” hivyo ukachelewesha ndoa kwa ajili ya maslahi mengine. Kwa nini?” Kwa sababu miadi na ndoa si kikomo cha safari zetu. Ni lango la kule hatimaye tunataka kwenda. “Kwa hiyo mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, na atashikamana kwa mke wake.”11

Jukumu lako sasa ni kuwa mstahiki kwa mtu unayetaka kumwoa. Kama unataka kuoa mwenye uchangamfu, anayevutia, mwaminifu, mwenye furaha, mchapa kazi, mtu wa kiroho, basi uwe mtu wa aina hiyo. Kama wewe ni mtu huyo na hujaoa bado, kuwa na subira. Msubirie Bwana. Nashuhudia kwamba Bwana anajua hamu zako na anakupenda kwa kujitolea kwako kwa imani Kwake. Ana mpango kwa ajili yako, iwe ni katika maisha haya ama yajayo. Silikiliza Roho Wake. “Usitafute kumshauri Bwana, lakini kupokea ushauri kutoka kwake.”12 Katika maisha haya au yajayo, ahadi zake zitatimizwa. “Kama umejitayarisha hutaogopa.”13

Kama hauna mali nyingi, usijali. Muumini wa ajabu wa Kanisa majuzi aliniambia, “Mimi sikuwalea watoto wangu kwa pesa; niliwalea kwa imani. Kuna ukweli mkuu katika hayo. Anza kufanya imani katika kila sehemu ya maisha yako. Kama hautafanya hivyo, utaugua kile ninachokiita “imani nyauka.” Nguvu hasa zinazohitajika kufanya imani yako zitafifia. Kwa hivyo fanya imani kila siku, na wewe atapata “nguvu kwa nguvu ... wakawa imara zaidi na imara katika imani ya Kristo.”14

Kuwa tayari kwa ndoa, hakikisheni kwamba mnastahili kupokea sakramenti na mnastahili kuwa na sifu ya hekalu. Nendeni hekaluni kila mara. Mhudumu katika Kanisa. Pamoja na miito ya Kanisa, fuateni mfano wa Mwokozi, ambaye kwa urahisi, “aliendelea kufanya mema.”15

Sasa, mnaweza kuwa na maswali ya dhati kuhusu chaguzi za huko mbele. Katika miaka ya ujana wangu, nilitafuta ushauri kutoka kwa wazazi wangu na kutoka kwa washauri waaminifu wanaoaminika. Mmoja alikuwa mwenye ukuhani; mwingine alikuwa mwalimu ambaye aliniamini. Wote waliniambia, “Kama unataka ushauri wangu, uwe tayari kuukubali. Mimi nilielewa hiyo ilimaanisha nini. Kwa maombi chagua wanasihi ambao wana usimamizi wa kweli kuhusu ufanisi wako wa kiroho. Uwe mwangalifu kuhusu kuchukuwa ushauri kutoka kwa rika lako. Kama unataka zaidi ya uliyonayo sasa, angalia juu, siyo kando kando!16

Kumbuka, hakuna anayeweza kufikia juu kwa niaba yenu. Bali imani yenu tu na maombi yatasababisha nyinyi kuwa na mabadiliko makubwa ya moyo. Uamuzi wenu tu kuwa watiifu unaweza kubadili maisha yenu. Kwa sababu ya dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi kwa ajili yako, uwezo upo ndani yako.17 Una wakala wako, una ushuhuda thabiti kama wewe ni mtiifu, na unaweza kumfuata Roho ambaye hukuongoza.

Hivi majuzi, kijana mtengeneza filamu alisema alihisi alikuwa sehemu ya “kizazi cha wapotevu”—kizazi “kinachotafuta matumaini na shangwe na ukamilifu, lakini kutafuta katika sehemu zote mbaya na kwa njia mbaya.”18

Katika fumbo la Mwokozi la mwana mpotevu, mwana alikuwa na baraka nyingi zikimsubiri, lakini kabla hajazidai, ilibidi angalie kwa makini maisha yake, chaguo zake, na hali zake. Muujiza ambao ulitokea baadaye umeelezewa katika maandiko kwa kishazi rahisi: “Alipozingatia moyoni mwake.”19 Acha niwatie moyo mzingatie moyoni mwenu? Katika Kanisa, wakati maamuzi ya muhimu lazima yafanywe, kila mara tunakuwa na mikutano ya baraza. Mikutano ya baraza ya familia inatumikia azma sawa. Mnaweza kutaka kuendesha kile nitaita “baraza binafsi.” Tumia muda kiasi peke yako. Fikiria kuhusu mambo yaliyo mbele. Jiulize: “Ni sehemu gani za maisha yangu ninazohitaji kuimarishwa ili kwamba niweze kuwaimarisha wengine? Wapi nataka niwe wapi mwaka mmoja kutoka sasa? Miaka miwili kutoka sasa? Ni chaguzi gani ninazohitaji kufanya kufika hapo?” Kumbuka tu, wewe ndiye rubani, na ndiyo unayeshikilia usukani. Ninashuhudia kwamba unapojitambua, Baba yako wa Mbinguni atakuja kwako. Kwa mikono ya kufariji ya Roho Yake Mtakatifu, Yeye atakuongoza.

Ninatoa ushuhuda wangu kwamba Mungu yu hai. Ninatoa ushuhuda wangu maalumu kwamba Mwokozi anawependa. “Je, si lazima sisi tuendelee katika kazi hii [Yake iliyo kuu]? Twende mbele na siyo nyuma.”20 Mnapomfuata Yeye, Atawaimarisha na kuwathibitisha. Yeye atawaleta hata kwenye nyumba yenu ya juu kabisa. Katika jina la Yesu Kristo, amina.