“Leo ni Siku ya Kushiriki Injili ya Mwokozi,” Liahona, Julai 2024.
Karibu kwenye Toleo Hili
Leo Ni Siku ya Kushiriki Injili ya Mwokozi
Rais Russell M. Nelson ametamka, “Hakujawahi kuwepo na kipindi kama cha sasa katika historia ya ulimwengu ambapo maarifa juu ya Mwokozi wetu ni muhimu zaidi kibinafsi na muhimu kwa kila nafsi ya mwanadamu” (“Ukweli Safi, Mafundisho Safi, na Ufunuo Safi,” Liahona, Nov. 2021, 6). Hii ndio sababu tunaukubali mwaliko na amri ya Mwokozi ya kushiriki injili Yake (ona Mathayo 28:19).
Hii ni kazi ya muhimu ambayo sote tunaweza kushiriki. Katika toleo hili Mzee Quentin L. Cook wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili anafundisha kwamba “fursa zipo kila mahali ili kuwasaidia wengine kuja kwa Kristo kwa kuonyesha upendo wetu, kushiriki imani zetu na kuwaalika kuungana nasi ili kufurahia shangwe ya injili ya Yesu Kristo” (ukurasa wa 4).
Tunayo shukrani kwa kila mvulana na msichana ambaye anahudumu katika misioni ya kufundisha au ya huduma, lakini kama ninavyoeleza katika makala yangu katika toleo hili, “Tunahitaji zaidi, wengi zaidi, kwenye mstari wa mbele—jeshi la wamisionari na waumini.”
“Leo ndiyo siku hiyo,” siku “ya sisi kuonyesha tabia na ujasiri na kushiriki injili ya Yesu Kristo” (ukurasa wa 40). Kadiri unavyojifunza jitihada za kimisionari za Amoni, Abishi na wengine katika Kitabu cha Mormoni mwezi huu, ninakualika kutafakari juu ya jinsi wewe unavyoweza kushiriki shangwe ya injili ya Mwokozi kwa wale wanaokuzunguka.
Mzee Eduardo Gavarret
Wa Sabini