Liahona
“Tafadhali Msaidie”
Julai 2024


““Tafadhali Msaidie,” Liahona, Julai 2024.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

“Tafadhali Msaidie”

Historia ya familia na kazi ya hekaluni kwa niaba ya wafu ilinisaidia nishinde hisia za kushindwa na upweke.

Picha
Hekalu la Manila Ufilipino

Picha ya Hekalu la Manila Ufilipino na Russell Sun De La Cruz

Siku moja kazini nilijisikia kuvunjika moyo na mpweke. Niliamini nimewaangusha mababu zangu kwa sababu ya makosa mengi niliyoyafanya. Nilimsihi Baba yangu wa Mbinguni anipe nguvu.

Wiki moja au mbili baadaye, dada mmoja alikuja kwangu baada ya ibada kanisani na kuniuliza kama nilikuwa Jenny Casama. Alijitambulisha kwangu kama Michelle (Mich) Bautista, mmoja wa washauri wetu wa kazi ya hekaluni na historia ya familia katika kata. Alieleza kwamba aliota ndoto ambapo katika ndoto hiyo wanawake watatu waliovalia mavazi meupe na majina yao ya ukoo ni Casama walikuja kwake kwa ajili ya msaada. Walimsihi Dada Bautista, “Tafadhali msaidie.”

Dada Mich alielewa kwamba wanawake hawa walikuwa wakimwomba amsaidie ndugu yao—mimi—kujifuza zaidi kuhusu kazi ya hekaluni na historia ya familia.

Dada Mich aliniambia, “Hebu tuone kama tunaweza kuwapata waanawake wale katika mti wa familia yako.”

Kwenye tovuti ya Familysearch, tuligundua kumbukumbu ya bibi yangu Damasa Casama, dada yake Emiliana Casama, na bibi wa mama yangu Eugenia Casama. Pasipo shaka yoyote, tulijua hawa walikuwa wale wanawake waliokuwa kwenye ile ndoto. Hisia tamu ya amani ikapita juu yangu, na nikahisi upendo wa mababu zangu ukifurika kwa wakati ule. Tulilia kwa sababu ya furaha tuliyojisikia mioyoni mwetu. Nilihisi walijali sana kuhusu mimi, na kwangu mimi, nilikuwa na upendo wa kina kwao.

Ndipo kisha nikatambua wajibu wangu wa kuwasaidia wao na mababu wengine kupokea ibada za hekaluni. Mababu zetu wamekuwa wakisubiri—wengine kwa muda mrefu—kwa sisi tulioko duniani kufanya ibada hizi takatifu kwa niaba yao.

Baadaye mwaka huo, nilibatizwa katika hekalu kwa niaba ya hawa mababu zangu watatu. Ninashuhudia juu ya uzuri wa kazi ya historia ya familia na nguvu iletayo katika maisha yangu.

Kama Rais Russell M. Nelson alivyosema: “Wakati kazi ya hekaluni na historia ya familia ina nguvu ya kuwabariki wale walio upande wa pili wa pazia, inayo nguvu iliyo sawa ya kuwabariki wale walio hai. Inayo nguvu yenye kutakasa juu ya wale ambao wamejiingiza kwenye kazi hiyo. Kwa hakika wanasaidia kuziinua familia zao.”

Ninajua kwamba Kanisa ni la kweli na kwamba hatuwezi kufanywa wakamilifu pasipo mababu zetu.

Chapisha