Liahona
Nairobi, Kenya
Julai 2024


“Nairobi, Kenya” Liahona, Julai 2024.

Kanisa Liko Hapa

Nairobi, Kenya

Picha
ramani ikiwa na duara kuzunguka Kenya
Picha
paa akiwa kwenye uwanja na majumba marefu upande wa nyuma

Watu wawili wa kwanza kujiunga na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho huko Kenya walibatizwa na kuthibitishwa mwaka 1979. Mwaka uliofuata wamisionari wawili wa kwanza, walikuwa wanandoa, waliwasili Kenya. Mwaka 1981, matawi mawili yalianzishwa, huko Nairobi na Kiboko. Leo, Kanisa nchini Kenya lina:

  • Waumini 17,430 (kwa makadirio)

  • Vigingi 2, kata na matawi 57, misioni 1

  • Hekalu 1 lililotangazwa (Nairobi)

Kupata Shangwe katika Bwana

Kama muumini mpya wa Kanisa, Gladys, Ondwari anapata shangwe katika injili hata wakati anapokabiliwa na majaribu: “Ninayo furaha sana! Bwana amenifungua macho katika wakati sahihi. Ninajua Yesu Kristo ndiye kimbilio langu mambo yanapokuwa magumu.”

Picha
mwanamke akiwa amevalia aproni akitabasamu

Picha na Lucy Stevenson Ewell

Zaidi kuhusu Kanisa nchini Kenya

  • Mvulana kutoka Kenya anahudumu misioni huko kaskazini magharibi ya Marekani, mahali ambapo anaweza kuwasaidia wakimbizi wa Kiafrika.

  • Wasifu mfupi na ushuhuda kutoka kwa msichana anayeishi nchini Kenya.

  • Mvulana anayeishi nchini Kenya anashiriki jinsi Kristo alivyomuimarisha kufanya mambo magumu.

  • Wanapoishi injili, waumini nchini Kenya wanatengeneza mbingu kutokana na msongo wa mambo ya ulimwengu.

  • Profesa wa historia ya Kanisa anasimulia ukuaji wa Kanisa katika Chyulu, Kenya.

Picha
mwonekano wa jiji la Nairobi

Katikati ya jiji la Nairobi. Kigingi cha kwanza cha Kanisa nchini Kenya kiliundwa huko Nairobi mnamo Sept. 9, 2001.

Picha
Mzee Sitati na mfanyakazi mmoja kwenye eneo la ujenzi wa hekalu

Wakati akihudumu kama Rais wa Eneo la Kati la Afrika, Mzee Joseph W. Sitati, raia wa Kenya, alizuru eneo la ujenzi wa Hekalu la Nairobi Kenya akiwa pamoja na viongozi wengine wa Kanisa mnamo Mei 21, 2022.

Picha
wanaume wawili wakiwa wamekaa pamoja

Kurithisha historia ya familia ni muhimu. Kuna vituo vitano vya FamilySearch nchini Kenya, na mawakala wenyeji huenda nje kukusanya historia hizo za simulizi ili ziweze kuhifadhiwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Picha
mama na wasichana wawili

Kanisa lilianza Kenya kwa waumini kukutana pamoja majumbani. Leo, kuna mikusanyiko zaidi ya 50 ya Watakatifu nchini Kenya.

Chapisha