2023
Unganika
Julai 2023


“Unganika,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2023.

Unganika

Aura K.

16, Nairobi, Kenya

Picha
msichana

Picha na Benson Arudo

Ninapenda kuoka. Ninapenda tabasamu ambazo huja kutokana na kuoka. Kila mtu anapenda vitafunwa vizuri. Wakati mmoja mama yangu aliacha viungo vyote vya mkate wa ndizi jikoni, lakini hakuwa akitarajia kutengeneza mkate huo.

Niliamua kuoka mkate huo kwa ajili yake. Punde niligundua kwamba mkate huo wa ndizi haukuwa kwa ajili yake. Badala yake, yeye alikuwa akiutayarisha ili kuwapatia wanafunzi wake. Mama yangu alifurahi sana kwa kumsaidia kwa njia hiyo.

Kazi ya umisionari ni kazi nyingine ninayoifurahia kuifanya! Baadhi ya shughuli za Kanisa ambazo nimezifurahia zimekuwa kuwapatia watu nakala za maandiko na kuwaimbia nyimbo za dini.

Wakati mwingine rafiki yangu alinikuta nikisoma gazeti la Liahona na akaniuliza kuhusu Kanisa. Nilimwelezea kuhusu toba na Upatanisho wa Yesu Kristo. Ailipendezwa sana, na nikampatia ile nakala ya Liahona.

Ninapenda kueneza injili kwa wengine ili nao wapate nafasi ya kujua zaidi kuhusu Baba wa Mbinguni.

Chapisha