“Mwana Mpotevu,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2023.
Mifano ya Mwokozi
Mwana Mpotevu
Mwana muasi anaomba urithi wake na anaondoka nyumbani.
Anapoteza kila kitu alichopewa na baba yake kwenye starehe.
Njaa inampiga, hivyo anafanya kazi ya kulisha nguruwe.
Siku moja anatambua kwamba anaweza kwenda nyumbani na kuomba msaada.
Anapofika nyumbani, anaomba kuwa mtumishi kwa familia yake, pasipo kuamini kuwa anastahili kutendewa kama mmoja wa wana wa baba yake tena.
Lakini baba yake anamsamehe mwana mpotevu na kumpokea kama mwanawe, na nyumba yote inasherehekea kurudi kwa yule mwana.
Kile Inachomaanisha
Mwana mpotevu anatuwakilisha sisi wakati tunapoasi dhidi ya Baba yetu wa Mbinguni. Lakini bila kujali tulikoenda au kitu tulichofanya, Baba wa Mbinguni anatutaka turudi nyumbani Kwake na kwenye injili ya Yesu Kristo.
Hatuhitaji kuwa wakamilifu. Tunapaswa kuwa wenye majuto na wanyenyekevu, tuje kwa Kristo, na tutubu. Mungu atatuvika mavazi ya utukufu na kutuonesha thamani yetu ya kweli.