2023
Siku Saba za Kushiriki
Julai 2023


“Siku Saba za Kushiriki,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai. 2023.

SikuSaba za Kushiriki

Unaweza kushiriki injili katika njia za kawaida na za asili kabisa. Uko tayari kwa changamoto hii?

Tunapozungumzia kuhusu kushiriki shuhuda zetu, mara nyingi tunafikiri kutoa shuhuda zetu katika mkutano wa sakramenti au kwenye fursa zingine rasmi. Lakini tumekuwa tukihimizwa “kutafuta fursa ya kuikuza imani yako katika njia za kawaida na za asili kabisa.”1

Katika changamoto hii hapa chini ya siku saba, unaweza kushiriki ushuhuda wako katika njia tofauti kila siku kwa wiki nzima. Unaweza kufanya mambo haya katika mpangilio wowote ule, au unaweza hata kuja na mawazo yako mwenyewe! Uko tayari kwa changamoto hii?

Picha
nyumba ya mkutano

Vielelezo na Emily Davis

Siku ya 1: Kanisani

Fikiria kutoa ushuhuda wako katika siku ya mkutano wa mfungo na ushuhuda kanisani kama hili ni jambo linalokufanya uhisi vizuri. Kama sivyo, unaweza pia kushiriki ushuhuda wako kanisani kwa kushiriki katika madarasa yako ya Jumapili na katika seminari. Maoni unayotoa huko yanaweza kuwainua wengine na kuimarisha shuhuda zao na wako pia.

Picha
marafiki

Siku ya 2: Marafiki

Ulijifunza nini kanisani Jumapili? Je, ulipenda kile mtu alichoshiriki katika mahubiri ya mkutano wa sakramenti au kwenye mjadala darasani kwako? Yawezekana wimbo wa ufunguzi ulikuwa mojawapo ya nyimbo zako pendwa. Mwambie rafiki yako juu ya hilo. Kisha waulize kuhusu wikiendi yao pia.

Picha
simu pamoja na mitandao ya kijamii

Siku ya 3: Mitandao ya Kijamii

Mitandao ya kijamii ni mahali pazuri pa kushiriki mambo ya kiroho kwa kawaida na kwa asili. Kwa siku hii ya changamoto, fikiria kushiriki posti kuhusu:

  • Mstari mmojawapo wa andiko ulipendalo.

  • Nukuu yenye kuinua kutoka kwenye mkutano mkuu.

  • Wazo la kiroho au uzoefu.

  • Kitu unachokipenda au unachoshukuru kuhusu Mwokozi.

  • Namna alivyokusaidia wewe hivi karibuni au sifa unayoipenda Kwake na kwa nini.

Picha
simu pamoja na video na ujumbe wa maandishi

Siku ya 4: Ujumbe wa Maandishi au Video

Tuma ujumbe wenye kuinua kwa rafiki kupitia maandishi na video. Ungeweza kushiriki hotuba ya mkutano unayodhani wanaweza kuipenda, waambie kitu unachoshukuru kuhusu wao, au shiriki kuhusu imani yako katika Yesu Kristo. Kwa mfano, yawezekana wakahitaji kujua kuhusu upendo wa Baba wa Mbinguni kwao. Unaweza pia mara zote kuwaambia wao kama mtu mmoja mmoja!

Picha
msichana akiwa na puto lenye umbo la moyo

Siku ya 5: Huduma

Unaweza kujiuliza jinsi kuwahudumia wengine kunavyoweza kuwa njia ya kushiriki ushuhuda wako. Mtume Paulo alimwambia Timotheo, “Uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi, na mwenendo, katika upendo, na imani, na usafi” (1 Timotheo 4:12). Hivyo unaweza kuonesha imani yako kupitia mfano wako, kwa kuwahudumia wengine kama vile ambavyo Mwokozi angewahudumia.

Picha
Vifaa vya Sanaa

Siku ya 6: Sanaa

Wakati mwingine watu wanatumia sanaa kama njia tofauti ya kushiriki mawazo na hisia zao. Unaweza kutumia picha ya kuchora, picha ya kuchonga, ufinyanzi, muziki, au aina nyingine ya sanaa ili kushiriki jinsi unavyohisi kuhusu Yesu Kristo na injili Yake.

Picha
vijana wakizungumza

Siku ya 7: Mazungumzo ya Kawaida

Usiogope kutaja imani yako katika vikao vya kawaida, kama vile ambavyo ungeshiriki mawazo yako yoyote mengine uliyo nayo kuhusu mada iliyopo.

Unaweza, hata hivyo, kuzungumzia kuhusu shughuli za Kanisa au maandiko uliyosoma hivi karibuni, lakini pia inaweza kuwa ya kawaida zaidi ya hivyo. Kwa mfano:

  • Kama unahisi kuvutiwa na mazingira ya asili, eleza shukrani zako kwa uumbaji wa Mungu kwa mtu mwingine.

  • Inawezekana ulipitia jambo zuri la kiroho hivi karibuni. Mwambie rafiki juu ya hilo kama siyo la binafsi sana.

  • Tafuta analojia za injili katika kitabu au sinema unayoipenda, na shiriki utambuzi wako.

Kawaida na ya asili

Unapopata njia tofauti tofauti za kushiriki imani yako, itakuwa rahisi zaidi na zaidi kwako kufanya hivyo. Unaweza kuhisi vibaya mwanzoni, lakini ni sawa tu! Kumbuka, ushuhuda wako peke yake tayari ni kitu cha asili kwako—ni sehemu ya wewe ulivyo. Kuushiriki inaweza kuwa ni asilia pia. Kile kinachohitajika ni kuuelezea kidogo kidogo kila siku.

Je! utashiriki vipi ushuhuda wako leo?

Chapisha