2023
Je, itakuwaje ikiwa mtu ananiambia kwamba sayansi haikubaliani na kitu tunachokiamini?
Julai 2023


“Je, itakuwaje ikiwa mtu ananiambia kwamba sayansi haikubaliani na kitu tunachokiamini?,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2023.

Kwenye Hoja

Je, itakuwaje ikiwa mtu ananiambia kwamba sayansi haikubaliani na kitu tunachokiamini

vyombo vya kisayansi

Rais Russell M. Nelson amefundisha: “Mungu ndiye chanzo cha ukweli wote. Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho linakumbatia ukweli wote ambao Mungu anaufikisha kwa watoto Wake, iwe wamejifunza kutoka katika maabara za kisayansi au umepokelewa moja kwa moja kwa ufunuo kutoka Kwake.” (“Ukweli ni Nini?” Mkutano mkuu wa Okt. 2022 [Liahona, Nov. 2022, 30]).

Ikiwa watu wanasema sayansi inakanganya ukweli wa injili, hapa kuna mambo ya kuweka akilini:

Unapaswa kupata ukweli. Pata kujua kile ambacho sayansi inadai (na kile isichodai), vile vile kile ambacho injili ya urejesho ya Yesu Kristo inadai (na kile isichodai). Weka kipaumbele katika kujifunza maandiko na maneno ya manabii.

Maarifa ya kiroho ni halisi. Sayansi ni mbinu ya kujifunza ukweli wa ulimwengu wa kimwili. Lakini kuna baadhi ya kweli Mungu anazotupatia kupitia ufunuo pekee. Unaweza kuwa na imani kwamba Roho Mtakatifu “anazungumza juu ya vitu kama vilivyo” (Yakobo 4:13).

Imani huhitaji subira. Maarifa ya kisayansi yanarekebishwa baada ya wakati. Wakati mwingine tunapaswa kusubiri tu sayansi ipate ukweli uliofunuliwa. Tunaweza kushikilia kweli pana zaidi wakati tukingojea maelezo ya kina yanapojazwa.