2023
Ninawezaje kuwa mfano kwa wanafamilia wanaotatizika kuishi mafundisho ya Yesu Kristo?
Julai 2023


“Ninawezaje kuwa mfano kwa wanafamilia wanaotatizika kuishi mafundisho ya Yesu Kristo?” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2023.

Maswali na Majibu

“Ninawezaje kuwa mfano kwa wanafamilia wanaotatizika kuishi mafundisho ya Yesu Kristo?”

Onesha, Hudumu, na Shiriki

Picha
msichana

“Ioneshe familia yako jinsi gani kuishi injili hukufanya uhisi furaha. Unaweza kuwahudumia na kushiriki uzoefu wako pamoja nao. Unaweza pia kuwaalika wamisionari kuwa na jioni ya nyumbani nyumbani kwako.”

Luciana M., 18, Mendoza, Argentina

Tafuta Kuelewa

Picha
msichana

“Baadhi ya washiriki wa familia yangu wamefanya baadhi ya mambo ambayo hayako sambamba na viwango vya Mungu. Jaribu kuelewa sababu zao kwa ajili ya kile wanachofanya. Hii haimaanishi wewe ufanye kile wanachokifanya. La muhimu zaidi, wapende bila kujali kile wanachofanya au wanachosema.

Melody E., 13, Texas, Marekani

Mfuate Mwokozi

Picha
msichana

“Mimi daima ninajaribu kuwa mfano kwa familia yangu kwa kuzungumza kuhusu mafundisho ya Kanisa. Daima ninajaribu kumuakisi Kristo kwangu mwenyewe. Ninajua kwamba kama ninamfuata Yeye, nitaweza kuwa mfano mwema kwa familia yangu na kusaidia kuleta nuru ya Kristo katika maisha yao.”

Adalia C., 19, Rio Grande do Sul, Brazili

Piga Miziki Yeye Kuinua

Picha
msichana

“Ninahakikisha ninazungukwa na vyombo vizuri vya habari ambavyo vinamleta Roho ndani ya nyumba yangu. Kupiga wimbo wa dini kwenye kinanda kunanisaidia nihisi furaha hata kama washiriki wa familia yangu wanatatizika. Endelea kumtegemea Mwokozi kwa ajili ya furaha na amani, hata kama wengine wanaokuzunguka hawafanyi hivyo.

Lauren B., 14, Maryland, Marekani

Wapende

“Huwezi kubadilisha chaguzi za washiriki wa familia yako sawa tu na wao wasivyoweza kubadili zako, lakini daima unaweza kuwapenda. Kristo alionesha upendo mwingi kwa watu ambao hawakukubaliana naye au hata hawakumpenda. Kila mtu ni mtoto wa Mungu, na kupitia upendo wako, wanaweza kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni.

Brooklyn D., 17, Utah, Marekani

Tafuta Kuona kama Kristo Anavyoona

Picha
mvulana

“Kuwa na upendo kama wa Kristo na kujaribu kuona zaidi ya udhaifu wao kunaweza kutusaidia tuelewe kile wanachopitia. Yesu Kristo anamwelewa kila mmoja wetu kikamilifu. Na tunaweza kuanza kuona na kuwasaidia wengine kama Yeye anavyofanya kama tutamwomba atuongoze.

John K., 17, Indiana, Marekani

Usihukumu

“Ninajifunza kuwapenda, kuwa mkarimu, na kutowahukumu.”

Logan C., 18, Utah, Marekani

Chapisha