2023
Kushikilia Ukweli
Julai 2023


“Kushikilia Ukweli,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2023.

Kushikilia Ukweli

Picha
msichana akiwa ameshikilia mpira wenye mwanga

Kielelezo na Ben Simonsen

Kwa mara ya kwanza nilipoona jengo la Kanisa, nilidhani kuwa ni hospitali. Lilikuwa safi sana na lenye ukimya. Niliipenda Injili ya Yesu Kristo wakati nilipohudhuria ibada kanisani.

Akina dada wamisionari walianza kunifundisha, na niliamua kubatizwa. Ilikuwa siku bora zaidi!

Nilitambulishwa kwenye injili na jirani yangu, ambaye ni mmisionari aliyemaliza muda wake na kurudi nyumbani. Alinipigia simu Jumapili moja asubuhi na kuniomba niende kanisani pamoja na familia yake. Mwanzoni, mama yangu aliniambia nisingeweza kwenda kwa sababu hatukuwa na pesa kwa ajili ya nauli. Nilipomwambia jirani yangu kuhusu hilo, alisema angenilipia, na mama yangu akaniruhusu.

Hata Wakati Tunapotembea Peke Yetu

Baada ya kubatizwa, nilipata nyakati nyingi ngumu na familia yangu. Wakati mwingine walinitaka nibaki nyumbani siku za Jumapili, lakini ningechagua kwenda Kanisani badala yake. Muda mwingi ilikuwa vigumu kujaribu kubaki katika njia ya agano.

Baadhi ya washiriki wa familia yangu wamekuwa wakipinga Kanisa na wameniambia kwamba nilifanya uchaguzi mbaya kujiunga. Wanaponiambia hili, maneno haya huja akilini mwangu: “Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni na Yeu Kristo wako hai. Ninajua kwamba Kanisa ni la kweli.” Mawazo haya yamenisaidia kushikilia ukweli huu.

Matendo Yetu Yanaweza Kugusa Maisha ya Wengine

Nilipotatizika kujua jinsi gani ya kulipa zaka, jirani yangu alinionesha jinsi ya kulipa. Sasa mama yangu anaponipa pesa ya matumizi, daima ninalipa zaka yangu. Mimi na familia yangu tunaona baraka kutokana na kulipa zaka. Familia yangu imeanza hata kunipa pesa zao ili nilipe kama zaka. Hilo limekuwa la kushangaza.

Muda mwingi mimi huenda kanisani peke yangu, lakini wakati mwingine mama yangu anajumuika nami. Mama yangu aliamua kujifunza zaidi kuhusu injili na anaona inaleta furaha, ingawa bado hajabatizwa.

Sala na Imani Zinabadilisha Mioyo

Nimeuona mkono wa Bwana katika maisha ya familia yangu wakati ninaposali kwa ajili yao na kuwaomba wengine wasali kwa ajili yao hekaluni. Washiriki wa familia yangu wamekuwa msaada zaidi, na sasa wananihimiza kwenda kanisani na kuwa mkweli kwa kile nilicho.

Babu yangu alifariki hivi karibuni, nilipata jina lake wakati nikifanya kazi ya historia ya familia. Nilimuuliza baba yangu ikiwa ninaweza kupeleka jina lake ili ibada zake zifanywe hekaluni. Alisema, “Fanya tu ilimradi ni jambo jema.”

Shangwe na Furaha ya Kweli

Kusoma maandiko na kujua kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo kumeniletea shangwe, furaha, amani, na faraja.

Ninajua kwamba kupitia dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi, ninaweza kuwa pamoja na Baba wa Mbinguni tena na kwamba familia yangu inaweza kuwa pamoja na mimi milele kama tutaunganishwa hekaluni siku moja.

Mwandishi anatoka Vanuatu na anaishi Fiji.

Chapisha