2023
Njia 4 za Kuwasaidia Marafiki walio katika Familia Ambazo Wengine Siyo Waumini
Julai 2023


“Njia 4 za Kuwasaidia Marafiki walio katika Familia Ambazo Wengine Siyo Waumini,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2023.

Msaadawa Kimaisha

Njia 4 za Kuwasaidia Marafiki walio katika Familia ambazo Wengine Siyo Waumini

Unaweza kumsaidia kila mtu ahisi kupendwa na kuthaminiwa kanisani bila kujali hali zao.

Familia zinakuja katika aina zote. Watu unaowaona kanisani, kwa mfano, yawezekana wanao washiriki wa familia ambao siyo waumini wa Kanisa au ambao wamechagua kuondoka Kanisani. Pasipo msaada wa familia, inaweza kuwa vigumu kwa watu kushiriki Kanisani, au hata kuhisi kuwa sehemu ya Kanisa.

Hapo ndipo wewe unapoingia!

Unaweza kuchukua nafasi muhimu katika kuzibariki aina zote za familia, katika aina zote za hali. Hapa kuna njia chache za jinsi unavyoweza kusaidia:

msichana akisali

Vielelezo na Oksana Grivina

Sali kwa ajili ya Njia za Kusaidia

Sali kujua jinsi unavyoweza kuwasaidia wale wote ambao wanakuja kanisani na familia zao. Kuwa tayari kuchukua hatua juu ya majibu unayopokea.

marafiki na familia

Ijue Familia

Kama inawezekana, jitahidi kuijua familia yote ya rafiki yako. Hii itakusaidia ujue ni msaada gani rafiki yako anao nyumbani na ni nini kinafanya kushiriki Kanisani kuwe vigumu kwao. Kadiri unavyoijua familia hiyo vizuri zaidi, unaweza kushawishika kusaidia katika njia mahususi ambazo zinahitajika.

vijana wakipanda ngazi

Hakikisha Unaishi Injili kwa Uthabiti

Watu wengi wanakuwa wenye kupendezwa na Kanisa wanapoona waumini wakiishi kile wanachoamini. Huwezi kujua nani anakuangalia. Unaweza kukamilisha mema mengi sana kwa kuishi tu injili. Kwa kufanya hivyo utabariki maisha yako na unaweza kusaidia kuleta nuru ya injili kwa wale wanaokuzunguka

watu mbalimbali

Kuwa Mkarimu Tu

Usidharau jinsi ukarimu rahisi unavyoweza kuleta tofauti kubwa. Kwa mfano:

Kama utamwona mtu amekaa pekee yake Kanisani, nenda ukae pembeni yake au mkaribishe akae na familia yako.

Kama hawawezi kufika kanisani au kwenye shughuli nyingine wao wenyewe, jitolee kuwapatia usafiri au waalike waje na familia yako.

Ni muhimu pia kuwajumuisha rafiki zako katika shughuli. Mwaliko wa shughuli ya kata au familia inaweza kuonekana ni jambo dogo, lakini inaweza kumsaidia rafiki achague kukaa karibu na Mwokozi na Kanisa Lake kama watahisi kujumuishwa.