2023
Zamani za Kufanywa Upya
Julai 2023


“Zamani za Kufanywa Upya,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Julai 2023.

Mstari juu ya Mstari

Zamani za Kufanywa Upya

Jifunze kile Mtume Petro alichowaambia watu kuhusu Urejesho.

Picha
Ono la Kwanza

Ono la Kwanza, na Walter Rane

nyakati za kuburudishwa

“Nyakati za kuburudishwa” Petro alizozizungumzia ni wakati ambapo Yesu Kristo atakuja tena. Baada ya Ujio wa Pili, “dunia itafanywa upya na kupokea utukufu wake wa kiparadiso” (Makala ya Imani 1:10).

zamani za kufanywa upya vitu vyote

“Zamani za kufanywa upya vitu vyote” ni wakati Urejesho wa Injili utakapofanyika. Wakati huo unajumuisha siku za mwisho (siku zetu!) na wakati Yesu Kristo anapokuja tena.

Urejesho inamaanisha kurudisha au kuleta kwa mara ya pili. Urejesho wa injili ulianza katika majira ya kuchipua ya mwaka 1820, wakati Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walipomtokea Joseph Smith. Hapo ndipo mambo mengi yalipoanza kurudishwa duniani, ikijumuisha ukweli safi wa Yesu Kristo, mamlaka ya ukuhani, na Kanisa.

manabii wake wote tangu ulimwengu uanze.

Tangu nyakati za kale, manabii wametabiri kwamba Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, angekuja duniani na kuwa Mwokozi wetu. Pia walitabiri kwamba Yesu Kristo angekuja mara ya pili.

Na manabii pia walitabiri kwamba kabla ya Mwokozi kuja tena, Yeye angerejesha injili Yake na Kanisa Lake duniani. Urejesho ambao manabii waliutabiri unatokea katika siku yetu.

Chapisha