2023
Wakati Chaguzi za Watu Wengine Zinapokuumiza
Julai 2023


“Wakati Chaguzi za Watu Wengine Zinapokuumiza,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2023.

Wakati Chaguzi za Watu Wengine Zinapokuumiza

Haya ni baadhi ya mambo ya kukumbukwa wakati watu wengine wanapotumia haki yao ya kujiamulia katika njia ambazo zinakuumiza wewe.

Picha
msichana akipitia uzoefu wa hisia hasi

Vielelezo na Shana Keegan

Unafanya tani nyingi za chaguzi kila siku—kipi cha kuvaa, nini cha kula kwa ajili ya kifungua kinywa, rafiki gani wa kuwa naye. Haki ya kujiamulia au uhuru wa kuchagua na kutenda, ni moja ya zawadi kubwa ambazo Mungu ametupatia.

Chaguzi zetu pia zina matokeo, na wakati mwingine chaguzi za watu wengine zinaweza kutuumiza. Kama umewahi kukwama kwa sababu ya kitu ambacho ndugu yako alifanya, utakuwa unajua jinsi ilivyo changamoto wakati watu wengine wanapotumia haki yao ya kujiamulia katika njia usizotaka!

Lakini wakati mwingine kuna hata mambo mabaya zaidi ambayo watu wanaweza kutumia haki yao ya kujiamulia kuyafanya. Watoto shuleni wanaweza kukuonea, au pengine mwanafamilia anaamua kuacha Kanisa. Kuna nyakati nyingi sana maisha yanaweza kuonekana siyo ya haki. Hata hivyo, unajitahidi kutumia haki yako ya kujiamulia kufanya chaguzi sahihi—kwa nini wao hawafanyi vivyo hivyo?

Bila shaka, wewe huwezi kuwadhibiti wengine. Lakini habari njema ni kwamba wewe mwenyewe unaweza kubadilika. Mkakati ni kubadili kile unachofokasi juu yake na kufanya chaguzi nzuri hata kama wengine hawafanyi hivyo.

Haya ni baadhi ya mambo ya kukumbukwa kuhusu kusonga mbele kwa imani, hata kama watu wengine wanatumia haki yao ya kujiamulia katika njia inayokuumiza wewe:

  1. Shetani alijaribu kuangamiza haki ya kujiamulia (ona Musa 4:3). Ingawa ni vigumu kuwaangalia wengine wakifanya chaguzi mbaya, wewe pia uko huru kufanya chaguzi nzuri za kumfuata Yesu Kristo na kuwa zaidi kama Yeye!

  2. Matendo yako yana athari. Kumbuka, “Tuko huru kuchagua, lakini hatuwezi kuchagua matokeo.”1 Kuona jinsi chaguzi za watu wengine zinavyokuathiri inaweza kuwa ukumbusho mzuri wa wewe kufanya chaguzi ambazo hazikuumizi wewe mwenyewe au wengine.

  3. Kila mtu anawajibika kwa chaguzi zake mwenyewe (ona Mafundisho na Maagano 101:78). Haupaswi kubeba mzigo wa hisia za wajibu wa kuwabadilisha watu wengine au chaguzi zao. Badala yake, wewe unaweza kufokasi katika kufanya maamuzi chanya na kumfuata Yesu Kristo.

  4. Unaweza kuchagua kuwa mkarimu. Mtu fulani anaweza kuwa mwonevu kwako, lakini wewe unaweza bado kuwa mkarimu kwao. Inahitaji ujasiri kuwa mkarimu kwa watu na kuwasamehe wanapokuwa siyo wakarimu kwako, lakini hivyo ndivyo hasa Yesu angekutaka ufanye (ona Luka 23:34).

  5. Unapaswa kufokasi juu ya kile ambacho unaweza kukidhibiti. Yawezekana ukashindwa kuwazuia wazazi wako wasitalikiane, kwa mfano, lakini unaweza kufokasi kwenye kubaki kwenye njia ya agano, ukiwasaidia ndugu zako, ukijifunza kuhusu uhusiano wenye afya, na kuweka malengo kwa familia yako ya baadaye. Chagua kugeuza changamoto zako kuwa fursa ya kukua na kujifunza.

  6. Unao utambulisho na kusudi la kiungu. Unapokumbuka utambulisho wako kama mtoto wa Mungu na kufokasi tena kwenye malengo yako katika maisha, unaweza kuona picha kubwa. Kufokasi kwenye kusudi lako na kuona kwamba changamoto hizi ni sehemu ndogo tu ya hadithi yako ya maisha kunaweza kukusaidia usonge mbele kwa imani.

  7. Kupitia imani katika Yesu Kristo, unaweza kupata amani binafsi, hata kama mambo yanayokuzunguka siyo ya amani. Rais Russell M. Nelson alisema, “Tunaweza kuhisi amani na shangwe ya kudumu, hata nyakati za misukosuko.”2 Maisha ni bahari yenye dhoruba, na ni rahisi kutamani kwamba Mungu angetuliza dhoruba hizo kwa ajili yetu. Lakini wakati mwingine badala ya kuifanya bahari itulie, Yeye anatutuliza sisi, mabaharia. Mgeukie Yeye ukiwa na matatizo yako, Naye atakusaidia.

Picha
msichana

Mungu alikupatia haki ya kujiamulia ili kwamba uweze kuchagua kumfuata Yeye na hivyo kuwa kama Yeye. Ufanyapo hivyo, kwa asili utajifunza kutokana na chaguzi na makosa yako mwenyewe na kutokana na chaguzi za wengine. Ingawa ni vigumu kuangalia watu wakifanya chaguzi ambazo zinakuumiza, unaweza kujifunza kutokana na uzoefu huo na kusonga mbele kwa lengo, imani na shangwe.

Chapisha