2023
Kusali ili Kupata Msaada Dhidi ya Waonevu
Julai 2023


“Kusali ili kupata Msaada dhidi ya Waonevu,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Julai 2023.

Misingi Imara

Kusali ili Kupata Msaada Dhidi ya Waonevu

Picha
vijana shuleni

Kielelezo na Jessica Parker

Wakati mwingine watu wanatuhukumu kwa kuwa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho na kwa kuwa tofauti. Mwaka jana nilionewa sana na watu shuleni. Lakini nilihisi msaada wa Mungu wakati wengine waliponisaidia nijitetee mwenyewe dhidi ya waonevu hao. Ilikuwa kama vile ngao ya ulinzi kutoka kwa Mungu.

Nilisali kwamba ningepata uwezo wa kuwasamehe watu walionionea. Nimewasamehe moyoni mwangu, na sasa ninatabasamu kwao na kuwasalimia ninapowaona.

Ninapenda kuwasaidia wengine, kama vile timu yangu ya soka, siyo kuwahukumu watu. Ninataka wengine waone picha kamili ya mimi ni nani na wengine ni nani.

Matthew H., Arizona, Marekani

Chapisha