Liahona
Je, Ungeweza Kuacha Nini ili Kumjua Mungu?
Julai 2024


“Je, Ungeweza Kuacha Nini ili Kumjua Mungu?,” Liahona, Julai 2024.

Njoo, Unifuate

Alma 22

Je, Ungeweza Kuacha Nini Ili Kumjua Mungu?

Picha
mwanamume akitembea ufukoni

Kuishi Injili mara nyingi inahitaji dhabihu. Baba wa Mbinguni anatutaka tuache mielekeo yetu ya asili ili tupokee kitu kilicho kikubwa zaidi: maarifa juu ya Mungu na baraka zisizolinganishwa na chochote ambazo Yeye hutoa.

Baba wa Mfalme Lamoni alionyesha utayari huu wa kutoa dhabihu wakati aliposali, “Kama yuko Mungu, na kama wewe ndiwe Mungu, nijulishe na Nitaacha dhambi zangu zote ili nikujue wewe, na kwamba niinuliwe kutoka kwa wafu, na niokolewe siku ya mwisho” (Alma 22:18; msisitizo umeongezwa).

Rais Russell M. Nelson alifundisha kwamba kuushinda ulimwengu na kusonga karibu zaidi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kunajumuisha “kukataa chochote ambacho kinamfukuza Roho” na “kuwa tayari ‘kuacha’ hata zile dhambi tuzipendazo.”

Baraka

Katika nyongeza kwenye baraka ambazo baba wa Mfalme Lamoni alizitafuta, kwa majina ufufuko na wokovu, Rais Nelson ameorodhesha baraka zaidi zinazokuja kutokana na juhudi za kuwa zaidi kama Yesu Kristo na kubaki katika njia ya agano. Hizi zinajumuisha:

  • Badiliko la moyo na asili

  • Hisani

  • Unyenyekevu

  • Utu wema

  • Ukarimu

  • Nidhamu binafsi

  • Amani

  • Kujiamini

  • Shangwe

  • Pumziko

  • Nguvu ya Kiroho

  • Ufunuo Binafsi

  • Ongezeko la imani

  • Huduma ya Malaika

  • Miujiza

Kama una wakati mgumu kutoa dhabihu dhambi fulani, usikate tamaa. Rais Nelson anatukumbusha kwamba “kuushinda ulimwengu hakika hakumaanishi kuwa wakamilifu katika maisha haya, wala haimaanishi kwamba matatizo yako yatayeyuka kichawi—kwa sababu hayatayeyuka. Na haimaanishi kwamba hautafanya dhambi. Lakini kuushinda ulimwengu kunamaanisha kwamba uwezo wako wa kupinga dhambi utaongezeka.”

Tunapoweka juhudi ya kuacha dhambi zetu kama baba wa Mfalme Lamoni, tutakuja kuona kwamba kumjua Mungu siku zote kunastahili dhabihu. Katika kufanya hivyo, maisha ya kila mmoja wetu yatakuwa kitu kikubwa zaidi kuliko ambavyo tungeyafanya yawe sisi wenyewe.

Chapisha