Liahona
Nafsi Yangu Ilitamani Kuwa Hapo
Julai 2024


“Nafsi Yangu Ilitamani Kuwa Hapo,” Liahona, Julai 2024.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Nafsi Yangu Ilitamani Kuwa Hapo

Hadithi pendwa ya maandiko ilikuja kama jibu kwa hamu yangu ya kuwa karibu na Baba yangu wa Mbinguni na Mwana Wake.

Picha
Ujio wa Pili wa Yesu Kristo

Ujio wa Pili, na Harry Anderson

Nilikuja hekaluni siku moja nikiwa na swali moyoni mwangu “Baba wa Mbinguni, ninaendeleaje katika injili?”

Mapungufu yangu yalionekana mengi hususani wiki hiyo. Kama Nefi, nilihisi kubeba mzigo wa dhambi ambazo kwa urahisi kabisa ulinilemea. Lakini, pia kama Nefi, nilijua katika nani nina tumaini. (Ona 2 Nefi 4:18–19.) Nilitumaini kutumia muda na Bwana katika nyumba Yake asubuhi ile kungenisaidia kuziba umbali niliokuwa ninauhisi.

Nilisikiliza kwa makini wakati wa kikao cha endaumenti na nikahisi shukrani kwa ajili ya nguvu na maarifa ambayo kikao kile kilitoa. Lakini nipokuwa naingia chumba cha selestia, moyo wangu bado nilihisi ni mzito. Je, ningewezaje kujua msimamo wangu kwa Bwana?

Nilikaa na kutafakari kwa dakika chache na kisha, nikihisi kukata tamaa, nilianza kusimama. Lakini kitu fulani kilinivuta nikae chini, kikinizamisha chini zaidi kwenye kochi. “Sitaki kuondoka,” niliwaza.

Nilitazama kuzunguka kile chumba na nikaona picha ya kuchora ya Yesu Kristo amezungukwa na malaika, mikono yake ikiwa imenyooshwa kunielekea mimi. Maneno ya lile andiko nilipendalo yakaja akilini mwangu: “Nafsi yangu ilitamani kuwa hapo” (ona Alma 36:22).

Mara kwa mara nimekuwa nikitafakari umuhimu wa mstari ule katika hadithi ya Alma. Mwanzoni, kwa sababu ya dhambi zake, wazo la kusimama mbele ya Mungu lilimjaza Alma “hofu isiyo elezeka” (Alma 36:14). Lakini baada ya kumgeukia Kristo, alimwona Mungu amezungukwa na malaika, na “nafsi yake ilitamani kuwa hapo.” Mwonekano huu wa kimaandiko umenivutia kila wakati. Juhudi ndogo za Alma za kutazama kwa Bwana zilileta matokeo makubwa kwenye moyo wake.

Niligundua kuwa sikuhisi kuondoka kwenye chumba cha selestia kwa sababu, kama Alma, nafsi yangu ilitamani kuwa hapo—kote hekaluni siku ile na mwishowe kuwa pamoja na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo katika nyumba yangu ya mbinguni. Roho Mtakatifu alitumia hadithi yangu ya kimaandiko niipendayo ili kuniambia kwamba Mungu aliujua moyo wangu. Nilikumbushwa kwamba licha ya mapungufu yangu, Bwana alipokea jitihada zangu za kuwa karibu na Yeye. Yeye alijua nilitamani kuwa hapo.

Chapisha