2021
Kadi za Historia ya Kanisa
Januari 2021


Kadi za Historia ya Kanisa

Jifunze kuhusu historia ya Urejesho! Kata kadi, zikunje kwa kufuata mistari ya nukta, na zifunge kwa kuzigundisha.

Picha
cutout cards of Emma and Joseph Smith

Emma Hale Smith

“Tunakwenda kufanya kitu kikubwa.”

Mihutasari ya Muungano wa Kike wa Usaidizi wa Akina Mama, 17 Machi. 1842.

  • Emma aliolewa na Joseph smith, na alikwenda na Joseph kuchukua mabamba kwenye Kilima Cumorah.

  • Wakati Joseph akitafsiri mabamba, Emma alikuwa wa kwanza kusaidia kuandika maneno.

  • Mungu alimuita ili aandae kitabu cha nyimbo kwa ajili ya Kanisa.

  • Alikuwa ni Rais wa kwanza wa Mungano wa Usaidizi wa Akina Mama.

Joseph Smith

“Nilijua, na nilijua kwamba Mungu alijua, na sikuweza kukataa.”

Joseph Smith Historia ya 1:25

  • Wakati Joseph akiwa na miaka 14, alisali ili kujua ni kanisa lipi lilikuwa la kweli. Baba wa Mbinguni na Yesu walimtokea.

  • Alisaidia kurejesha Kanisa la Yesu Kristo.

  • Alitafsiri mabamba ya dhahabu ili kwamba leo hii tuweze kusoma Kitabu cha Mormoni.

  • Mungu alimpa ufunuo (jumbe). Zimeandikwa katika Mafundisho na Maagano.

1804–1879

1805–1844

Vielelezo na Brooke Smart

Chapisha