2021
Ninawapenda
Januari 2021


Ujumbe Kutoka kwa Nabii

Ninawapenda

Imetoholewa kutoka “Restoration Conversation with President Russell M. Nelson,” Video Collection, Gospel Media library

Picha
President Nelson talking with children

Rais Nelson alikutana na baadhi ya watoto wa Msingi katika nyumba iliyojengwa kwa magogo huko Palmyra, New York, Marekani. Inaonekana kama nyumba ambapo Joseph smith aliishi wakati alipopata Ono la Kwanza. Hapa ni baadhi ya vitu ambavyo Rais Nelson alivishiriki pamoja na watoto.

Watoto Wote wa Mungu

Si muhimu wapi ulizaliwa au unapeperusha bendera gani au lugha gani unayozungumza. Sote tu watoto wa Baba wa Mbinguni, na tutakua kuja kuwa kama Yeye.

Juhudi na Tuzo

Kuwa nabii kunahitaji kazi kubwa sana na kujifunza sana. Kila kitu kinachohusiana na kuwa kama Mwokozi huhitaji juhudi. Wakati Mungu alipotaka kumpa Musa Amri Kumi, alimwambia Musa aende wapi? Juu kwenye kilele cha mlima Sinai. Kwa hivyo Musa alilazimika kutembea hadi juu ya kilele cha mlima huo ili kupata Amri Kumi. Bwana anapenda juhudi, kwa sababu juhudi huleta tuzo ambazo haziwezi kuja bila hiyo.

Familia ya Nabii

Sisi tu wazazi wa watoto kumi, mabinti wazuri tisa, na mvulana mmoja. Wawili kati ya hao wanaishi mbinguni sasa. Walikuwa na maisha mafupi hapa duniani, na wanashangilia kwa ajili yetu mbinguni. Tumeunganishwa katika ndoa ya hekaluni, ambayo humaanisha kwamba tutakuwa pamoja milele baada ya kuwa na sehemu yetu ndogo hapa duniani.

Kiambata cha Furaha

Maandiko ni kama kitabu cha mapishi. Kama huna kitabu cha mapishi, na ukaanza tu kuchanganya unga na maziwa na mayai, unaweza usiwe na keki nzuri. Mungu ametupatia kiambata kwa ajili ya furaha, na kinaitwa amri.

Neno amri linaonekana kama shuruti, kama vile tunaambiwa nini cha kufanya. Lakini ni njia fupi ya kujifunza. Kwa mfano, alituamuru sisi kutokunywa vilevi wala kuvuta sigara na vitu vingine vyenye madhara. Kwa nini? Ili kwamba uishi muda mrefu na kuwa na furaha zaidi. Je, mnadhani ningeishi miaka 95 kama ningekuwa navuta sigara na kunywa vilevi? Hapana. Na nina furaha. Na ninaweza kucheza mchezo wa kuteleza kwenye theluji pamoja na wajukuu zangu.

Kitu cha Kupendeza

Toba humaanisha kwamba kila siku, tunajaribu zaidi a kufanya zaidi kuwa kama Bwana Yesu Kristo. Bado ninatubu. Kila siku ninajaribu kujifunza zaidi na kuwa zaidi kama ambavyo Bwana angelipenda niwe. Na hiyo si adhabu. Ni fursa ya kupendeza. Kila siku asubuhi ninashuka kitandani na kusema, “O, kitu kizuri kinakwenda kutokea leo hii! Ninakwenda kuwa zaidi kama Yesu.” ●

Chapisha