2021
Taxi Moja Tu
Januari 2021


Taxi Moja Tu

Mwandishi anaishi Carolina ya Kaskazini, Marekani.

“Tusaidie kupata angalau taxi moja tu ili kwamba tuweze kufika kanisani leo,” wasichana walisali.

“Mara zote nakuwa na hisia za furaha pale ninapokwenda kanisani” (Kitabu cha Nyimbo za watoto, 157).

Tukio hili lilitokea huko Cantabria, Hispania.

Picha
two girls holding umbrella

“Je, tutafikaje Kanisani leo?” Peppa, dada mdogo wa Ellie, aliuliza. “Kuna mvua kubwa!”

“Usiwe na wasiwasi, Ellie alisema. “Sisi ni mashujaa!”

Ellie alimsaidia Peppa kufunga vifungo vya koti lake. Kisha akavaa viatu vyake vya kutembelea kwenye mvua.

Ellie na Peppa walitoka nje pamoja na Mama na Baba. Mvua ilikuwa ikinyesha kuliko kawaida. Upepo uliigeuza miamvuli yao ndani nje. Ellie hakuhisi kuwa shujaa tena.

“Tunapaswa kufanya nini?” Ellie aliuliza. Kulikuwa na upepo mkali kiasi cha kushindwa kwenda kwenye basi.

“Tutachukua taxi badala yake,” Baba alisema.

“Wazo zuri,” Mama alisema. “Twendeni!”

Waliembea kwenye mtaa uliofurika maji. Hakuna taxi wala magari yaliyopita. Hata panadería (duka la mikate) lilikuwa limefungwa.

Hatimaye waliona mahali ambapo taxi zilisimama kusubiri kuchukua watu. Lakini maegesho ya kwanza ya taxi yalikuwa tupu.

“Jamani!” Peppa alisema.

Está bien. Ni SAWA,” alisema Ellie. “Kunaweza kuweko nyingine. Lakini hatuioni kwa sasa.”

Walisonga karibu zaidi. yaliyofuata yalikuwa wazi pia.

“Sasa inakuwaje?” aliuliza Peppa.

“Ninajua,” Ellie alisema. “Ngoja tusali.”

Wasichana walisali kwa sauti ya chini. Baba wa Mbinguni tafadhali tusaidie kupata taxi moja tu ili kwamba tuweze kufika kanisani leo. Tunajaribu kuchagua kilicho sahihi, na mvua hii inafanya iwe vigumu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.” Ellie alikuwa bado anajifunza Kihispania, kwa hivyo alichanganya Kiingereza na Kihispania pamoja.

Wakatembea kidogo zaidi. Eneo la tatu la maegesho lilikuwa wazi pia.

“Labda tugeuke na kurudi nyumbani,” Baba alisema kwa sauti katika upepo.

“Miguu yetu imeloa!” Mama alisema.

“Acha twende kidogo zaidi,” alisema Ellie. “Tunahitaji taxi moja tu.”

Sasa wangeweza kuliona eneo la mwisho la maegesho.

Pale, ikiwa na taa ya kijani inayowaka, ilikuwa ni taxi!

Ellie na Peppa walirukia ndani ya taxi. Mama aliwasidia kunyoosha nywele zao. “Samahani kwa kulowanisha viti vyako,” Baba alimwambia dereva.

Walifika kanisani na kuwasalimu marafiki zao kwa besos na abrazos (mabusu na kumbatio).

“Siwezi kuamini tulipata taxi,” Mama alisema. “bahati iliyoje!

“Haikuwa bahati,” Ellie alisema. “Peppa na mimi tulisali kwamba Baba wa Mbinguni angetusaidia kufika kanisani. Na alisikiliza!” ●

Picha
Friend Magazine, 2021/01-02 Jan/Feb

Vielelezo na Patricia Geis

Chapisha