2021
Unaweza Kusaidia Kama Yesu!
Januari 2021


Mwaliko wa Mikono Saidizi

Unaweza Kusaidia Kama Yesu!

Picha
Jesus with children

Wakati Kristo akiwa duniani, Aliwasaidia wote Aliowaona. Aliwalisha wale waliokuwa na njaa. Aliwafariji wale wenye huzuni. Alimfundisha kila mmoja injili Yake. Yesu alituamuru tumfuate Yeye. Wakati tunapobatizwa, tunaahidia kujaribu kufanya Alichokifanya.

Leo hii watu wengi ulimwenguni wanahitaji msaada wetu. Baadhi ni wapweke. Baadhi wana njaa. Baadhi wamelazimika kuacha nyumba zao. Baadhi bado hawajaisikia injili. Kila mmoja wetu anaweza kufanya kitu fulani ili kusaidia.

Kile Mikono Yako Saidizi Inachoweza Kufanya

Watoto wanaweza kubadili ulimwengu kwa mioyo yao yenye upendo na mikono saidizi. Takribani miaka 100 iliyopita, watoto wa Msingi walisaidia kujenga hospitali huko Jijini Salt Lake, Utaha, Marekani. Kila wiki, walileta fedha kwa ajili ya hospitali mpya. Wakati ilipofunguliwa mnamo 1922, iliitwa Primary Children’s Hospital. Hiyo ni kwa sababu watoto walisaidia kuijenga, kidogo kidogo!

Wakati unapotazama mazingira yanayokuzunguka, utaona watu wengi ambao unaweza kuwasaidia. Unaweza kushiriki injili kupitia jinsi unavyoishi na kuwahudumia wengine. Unaweza kuwasaidia kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni.

Mwaliko wa Kusaidia

Mwaka huu tunawaalika kutumia mioyo yenu yenye upendo na mikono saidizi kuwasaidia wengine. Hisia za furaha unazokuwa nazo wakati unapomsaidia mwingine huja kutoka kwa Roho Mtakatifu. Zinakufanya ujue kwamba Baba wa Mbinguni anafurahishwa sana na juhudi zako!

Picha
pictures of children helping

Vielelezo na Liz Brizzi

Chapisha