2021
Yesu Aliwaona Wengine
Januari 2021


Kusaidia Kama Alivyofanya Yesu

Yesu Aliwaona Wengine

Picha
Jesus helping woman

Yesu mara zote aliwaona watu waliokuwa na uhitaji. Siku moja alikuwa katika umati mkubwa wa watu.

Mwanamke katika umati alikuwa ameugua kwa muda wa miaka 12. Alikuwa na imani kwamba Yesu angeweza kumponya. Hivyo alisonga na kugusa pindo la joho lake wakati Akipita.

Yesu alimuona yule mwanamke. Alisimama kumfariji. Mwanamke yule aliponywa kwa nguvu za Yesu.

Wakati wa COVID, niliwasiliana na marafiki zangu kuhakikisha kwamba walikuwa SALAMA na niliwasalimu kwa tabasamu la kutia moyo pale tulipozungumza pamoja kupitia mtandao. Nilitumia mikono yangu kusaidia shughuli za nyumbani na kuwasaidia wengine wenye uhitaji.

Blaine H., miaka 11, Ras Al Khaimah, Muungano wa Falme za Kiarabu

Picha
cutout challenge card

Vielelezo na Simini Blocker

Chapisha