2021
Kutana na Stella Kutoka Ghana
Januari 2021


Mikono Saidizi Ulimwenguni kote

Kutana na Stella Kutoka Ghana

Kutana na watoto wa Msingi wakiwasaidia wengine, kama Yesu alivyofanya.

Picha
brother and sister reading scriptures together

Yote kuhusu Stella

Miaka: 11

Kutoka: Ghana

Lugha: Kiingereza na Kitwi

Familia: Mama, Baba, na Kaka, Yaw

Malengo na ndoto: 1) kutumikia misheni, kama mama yake. 2) Kuolewa hekaluni. 3) Kuwa mwanamitindo

Stella akisoma maandiko pamoja na kaka yake.

Mikono Saidizi ya Stella

Karibu kila siku, unaweza kumkuta Stella na familia yake wakimtembelea mmiliki wa nyumba wanayoishi. Hawana undungu naye, lakini Stella na kaka yake wanamuita “Bibi Cecilia.” Stella anasema, “Bibi Cecilia ana miaka 83, na hana watoto wake wa kuzaa.” Stella na familia yake waligundua alihitaji msaada na wakaamua “kumuasili.”

Stella mara zote hutoa msaada kwa kufagia na kudeki sakafu ya Bibi Cecilia. Kuwa na nyumba safi ni njia muhimu ya kuwa mwenye afya. Hivyo Stella anafanya kitu ambacho kwa hakika humsaidia Bibi Cecilia. “Yesu Kristo aliwatumikia wengine,” anasema stella, “hivyo hilo hunipa msukumo wa kumtumikia Bibi Cecilia. Ninajua kwamba Yesu Kristo na Baba Yake wanafurahi pale ninapotumikia.” ●

Mapendeleo ya Stella

Sehemu: Hekalu la Accra Ghana (“Ni kama Mbingu hapa duniani.”)

Hadithi kuhusu Yesu: “Wakati alipolisha umati kwa samaki wawili na mikate mitano.”

Nyimbo za Msingi: Called to Serve” na “A Child’s Prayer” (“Zinanipa nguvu ya kupenda na kutumikia.”)

Chakula: fufu (mboga zilizosagwa pamoja na mihogo) pamoja na mchuzi na nyama ya mbuzi

Rangi: Manjano

Somo shuleni: sanaa ya ubunifu

Chapisha