2021
Marafiki Wapendwa
Januari 2021


Ujumbe Kutoka kwa Urais wa Kwanza

Marafiki Zetu Wapendwa Wadogo,

Picha
Primary children in Ghana holding up Friend magazines

Mwezi huu jarida la Rafiki linasherehekea mwaka wake wa 50 tangu kuanzishwa—na mwanzo mpya. Awali Jarida la Rafiki liliwafikia watoto wanaozungumza Kiingereza pekee. Sasa litakuwa likipatikana kwa watoto katika lugha 48 ulimwenguni kote. Tumaini letu ni kwamba kila mtoto wa Msingi anaweza kufurahia jarida la Rafiki nyumbani mwao na kulishiriki na wengine.

Kote ulimwenguni, watoto wa Msingi kama ninyi wanajaribu kumfuata Yesu. Kila mmoja ni mtoto mwenye thamani wa Mungu. Wakati usomapo jarida la Rafiki, utapata kuwajua marafiki hawa. Utajifunza kuhusu injili ya urejesho. Na utahisi ukaribu zaidi kwa Rafiki yako wa kweli, Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Kwa moyo wa dhati,

Urais wa Kwanza

Mchezo wa Kutafuta Bendera

Tafuta ukurasa kutoka kwenye nchi hizi tofauti. Kisha ziondoe bendera hapa chini!

  • Ghana

  • Korea ya Kusini

  • Kanada

  • Hispania

  • Ujerumani

  • Benin

  • Ajentina

  • Mexico

Wapi Tunasoma Jarida la Rafiki

Watoto hawa kutoka Ghana wamebeba nakala zao za jarida la Rafiki. Tutumie picha yako au darasa lako la Msingi mkiwa mmebeba jarida la Rafiki. Hakikisha unajumuisha ruhusa kutoka kwa mzazi (tazama jalada la nyuma).

Vielelezo na Adobestock.com

Chapisha