Onyesha na Eleza
Watoto wa Msingi huko Texas, Marekani, walitengeneza ubao wa dondoo ya Mwokozi akitokea, na kila mmoja kwenye Msingi akisimama kumzunguka Yeye. Hii humsadia kila mmoja kuhisi kuwa karibu na Yeye.
Habari, kutoka Msingi yetu huko Dakar, Senegal!
Nilikwenda kwenye matembezi ya kuokota na baba yangu na kukusanya vipande 322 vya takataka! Ilikuwa vizuri kufanya maeneo yetu ya jirani kuwa safi na nadhifu kwa ajili ya wengine kufurahia.
Sam D., miaka 8, Suffolk, Uingereza
Ubatizo wangu hunisaidia kukumbuka maagano muhimu niliyofanya na Baba wa Mbinguni. Ninajaribu kufuata amri Zake na kuwa binti na mfuasi mzuri.
Demmi E., miaka 9, Jiji la Mexico, Mexico
Wakati kulipozuka moto wa porini huko Australia, nilifunga kwa ajili ya wanyama waliokuwa hatarini. Tulisali kila usiku kwa ajili ya wazima moto kwamba Bwana angewalinda. Nilihisi furaha wakati Mama aliponiambia moto ulikuwa unazimika. Ninajua Baba wa Mbinguni hutusikia pale tunapofunga na kusali.
Lincoln B., miaka 9, Victoria, Australia
Nina marafiki wengi shuleni, na huwa tuna wakati mzuri. Siku moja nilimuona msichana mmoja akiwa mwenyewe, na nilitaka kuwa rafiki yake. Nilijua lilikuwa ni jambo sahihi kwa sababu thamni ya nafsi ni kuu mbele za Bwana.
Tatiana L., miaka 6, Sacatepéquez, Guatemala
Nilikuwa nikiogelea pamoja na familia yangu na nikagundua kuna mvulana alikuwa akihangaika majini. Nilikwenda na kumsaidia. Kaka yake mkubwa aliniambia kwamba nilikuwa shujaa kwa kusaidia. Baadaye, nilimhisi Roho Mtakatifu.
Christian M., miaka 9, Utah, Marekani