Ndoto kwa ajili ya Dieter
Imetoholewa kutoka kwa Mzee Dieter F. Uchtdorf, “Call for Heroes!” (BYU-Pathway Worldwide devotional, tarehe 14 Julai, 2020, byupathway.org/devotionals).
Alipokuwa mvulana, Mzee Dieter F. Uchtdorf alipenda kutazama ndege. Alifikiria wakati fulani kuendesha moja ya ndege hizo kubwa.
Siku moja, ningependa kuwa rubani.
Lakini familia ya Dieter haikuwa na pesa za kutosha. Walikuwa wakimbizi na walihitajika kuondoka nyumbani kwao mara mbili kwenda kwenye nchi ya ugenini.
Huku watoto wengine wakicheza, Dieter alifanya kazi kama mwasilishaji ili kuisaidia familia yake.
Wakati mwingine alihisi kuwa ndoto yake haikuwezekana!
Lakini alipoendelea kukua, Dieter alijitahidi kutimiza ndoto zake. Alikuwa na imani ya kwamba Baba wa Mbinguni angemsaidia.
Alijiunga na jeshi la angani na kupata mafunzo ya kuwa rubani bora kadiri ambavyo angeweza kuwa.
Mwishowe, alitimiza ndoto yake. Aliendesha ndege kubwa kwa miaka mingi!
Labda unajiuliza ikiwa ndoto zako zinaweza kutimia pia.
Huenda isiwe rahisi, lakini unaweza kuzitimiza.
Huenda ukakumbana na changamoto, lakini zinaweza kukufanya kuwa imara zaidi. Mungu yuko nawe kila hatua kwenye safari yako!
“Tia bidii. Kuwa na imani. Kuwa na tumaini. Mtumainie Mungu. Ukitekeleza wajibu wako, mambo yatakuwa sawa.”