Kadi za Historia ya Kanisa
Kata kadi, zikunje kwa kufuata mistari ya nukta kisha zifunge kwa kuzigundisha.
Jane Manning James
1822–1908
“Tulienda … tukifurahia, tukiimba nyimbo za kanisa na kumshukuru Mungu.”
Kutoka kwa James Goldberg, “The Autobiography of Jane Manning James,” Historia ya Kanisa, tarehe 11 Desemba, 2013, history.ChurchofJesusChrist.org.
-
Alijiunga na Kanisa huko Connecticut, Marekani.
-
Familia yake ilitembea zaidi ya maili 800 (kilomita 1287) ili kujiunga na Watakatifu huko Nauvoo. Wakati miguu yao ilipotoka damu, waliomba kuponywa na Mungu akajibu maombi yao.
-
Joseph Smith alisema alikuwa na imani kubwa.
-
Hata ingawa alikabiliwa na changamoto nyingi, alikuwa mwaminifu katika injili maisha yake yote.
Parley P. Pratt
1807–1857
“Roho wa Bwana alikuwa juu yangu na nilijua … Kitabu cha [Mormoni] kilikuwa cha kweli.”
Autobiography of Parley P. Pratt (1938), 38.
-
Wakati aliposoma Kitabu cha Mormoni kwa mara ya kwanza, hakuweza kuacha. Alikisoma mchana wote na usiku wote.
-
Alitumikia misioni nchini Kanada, Uingereza, Chile na visiwa katika Pasifiki Kusini.
-
Aliandika nyimbo za Kanisa ambazo bado tunaziimba leo, kama vile “Jesus, Once of Humble Birth” (Wimbo, nambari 196).
-
Alikuwa mmoja wa Mitume wa kwanza walioitwa katika Kanisa lililorejeshwa.