2021
Mchezo wa Ubao Juu ya Mpango wa wokovu
Julai/Agosti 2021


Mchezo wa Ubao Juu ya Mpango wa wokovu

Picha
Friend, July 2021 Tier 2

Cheza mchezo huu ili ujifunze kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni. Tumia maharage au sarafu kama vipande vya mchezo. Kwa kila zamu, bingirisha kete au uchague nambari na usogeze kipande kilicho na nafasi nyingi. Wakati mtu wa kwanza anapoipita nyota, soma kiputo. Wakati mwingine anapoipita nyota hiyo, fanya shughuli.

  • Maisha kabla ya kuja duniani: Tuliishi pamoja na wazazi wetu wa mbinguni. Tulichagua kumfuata Yesu Kristo na kuja duniani.

    Imbeni “I Lived in Heaven” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 4).

  • Dunia: Tulikuja duniani kupata mwili, kujifunza na kukua. Tunaweza kuchagua kati ya mema na mabaya.

    Soma Alma 34:32.

  • Upatanisho wa Kristo: Yesu Kristo alikuja duniani na kuishi maisha makamilifu. Anajua machungu yetu. Alilipia adhabu ya dhambi zetu ili tutubu.

    Imbeni “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35).

  • Ulimwengu wa roho: Baada ya kuaga dunia, roho zetu huendelea kuishi. Watu ambao hawakujifunza kuhusu injili duniani wanaweza kujifunza kuihusu huko.

    Soma Alma 40:11.

  • Ufufuko: Kwa sababu Yesu alifufuka kutoka kwa wafu, sisi sote tutaishi tena! Miili na roho zetu zitarudi pamoja.

    Imbeni “Did Jesus Really Live Again?” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64).

  • Ufalme wa selestia: Kwa sababu ya Yesu Kristo, tunaweza kuwa kama Baba yetu wa Mbinguni na kuishi na familia zetu milele.

    Soma Mafundisho na Maagano 76:70.

Chapisha