2021
Pichi Moja kwa Wakati
Julai/Agosti 2021


Rafiki kwa Rafiki

Pichi Moja kwa Wakati

Kutoka kwenye mahojiano na Amber Healey

Picha
girl picking a peach

Nilipokuwa msichana mdogo, wazazi wangu walinichukua mimi na dada yangu na kutupeleka kwenye shamba la matunda linalomilikiwa na Kanisa. Tulikuwepo hapo kusaidia kuchuma pichi. Tulipanda ngazi ndefu na kufika kupitia majani manene ili kuchuma pichi mitini.

Mwanzoni, tulikuwa na furaha kubwa. Lakini baadaye sufi zilizokuwa kwenye matunda zilifanya mikono yetu iume! Tulimwambia mama yetu, “Hatutaki tena kufanya shughuli hii. Tunataka kuacha.”

Mama yangu alituuliza ikiwa tulijua kule ambako pichi zote zilienda. Tuliposema hatujui, alituelezea.

Picha
family eating together

“Kila moja ya pichi hizi hupelekwa kwenye jengo ambapo watu wa kujitolea huziweka kwenye makopo. Kisha makopo hayo yanapewa watu wanaohitaji chakula. Kila mwaka Kanisa linatoa mchango wa maelfu ya makopo ya chakula.”

Ghafla, mimi na dada yangu tuliacha kuwa na wasiwasi kuhusu mikono yetu iliyouma. Tulikuwa tukiwasaidia watu waliohitaji chakula! Baada ya hayo, tulifurahia kupanda ngazi na kuchuma matunda ya rangi ya chungwa yenye sufi.

Mwaka huu tumekuomba ushiriki katika mwaliko wa Mikono Saidizi (tazama Januari 2021 Rafiki). Kuwatumikia wengine jinsi Kristo alivyotumikia ni moja ya vitu muhimu unavyoweza kufanya. Watoto wana njia maalum ya kutambua wale walio na mahitaji na kujitolea kusaidia. Kitendo kidogo cha utumishi huenda kisionekane kuwa kikubwa zaidi mara ya kwanza. Lakini ikiwa watoto wote kote duniani watatafuta njia za kutumikia, wataongeza kwenye vitu vinavyovutia!

Picha
Friend, July 2021 Tier 2

Vielelezo na Toby Newsome

Chapisha