Julai/Agosti 2021 Marafiki WapendwaUkurasa huu unajumuisha barua kutoka kwa wafanyakazi na mawasilisho kutoka kwa watoto kuhusu jinsi wanavyosoma gazeti la Rafiki. Dallin H. OaksKuwa MkarimuRais Oaks anasimulia hadithi kuhusu mvulana mkimbizi anayefanyiwa utani kwa kuwa tofauti. Anawahimiza watoto kuwa wakarimu. Imetoholewa kutoka kwenye hotuba ya mkutano mkuu. Haley YanceyChai au Sharubati ya Embe?Chung anafanya uamuzi wa kunywa sharubati kwa sababu chai ni kinyume cha Neno la Hekima. Rafiki yake, Jiro, anamsaidia kusimama pale anaposhindwa, hata ingawa Jiro si muumini wa Kanisa. Kutana na Eta kutoka Samoa ya AmerikaKutana na msichana kutoka Samoa ya Amerika anayesaidia kama Yesu. Yesu Alishiriki na WengineYesu aliwagawia wanafunzi wake mkate na samaki na kuwaambia wawasaidie wengine. Weka lengo la kumgawia mtu mwingine. Matukio katika Samoa ya Amerika Pamoja na Margo na PaoloJifunze kuhusu Samoa ya Amerika na kubali changamoto ya mwezi huu ya Mikono Saidizi. Charlotte LarcabalNdoto kwa ajili ya DieterHadithi ya jopo inayoelezea safari ya Mzee Dieter F. Uchtdorf ya kuwa rubani wa ndege na jinsi watoto wanavyoweza kuwa chochote wanachotaka kuwa. Sharon EubankPichi Moja kwa WakatiDada Sharon Eubank, mshauri wa kwanza katika urais mkuu wa Muungano wa Usaidzi wa Akina Mama, anazungumzia mawazo na hisia zake kuhusu mwaliko wa Mikono Saidizi. Pia anashiriki hadithi kuhusu kile alichojifunza alipokuwa akichuma pichi na familia yake akiwa msichana mdogo. Nahisi Upendo wa Mwokozi WanguToleo lililorahisishwa la wimbo kutoka kwenye Kitabu cha Nyimbo za Watoto. Richard M. RomneyPishi Jipya la WinfredWinfred anajifunza kuwa kuwatumikia wengine humsaidia kuwa na furaha. Mchezo wa Ubao Juu ya Mpango wa wokovuMchezo ulioundwa ili kuwafunza watoto kuhusu mpango wa wokovu na kuwahimiza kuchagua mema ili kufikia ufalme wa selestia. Onyesha na UsemeMawasilisho kutoka kwa watoto kote duniani yakizungumzia uzoefu binafsi katika mada kuanzia ubatizo hadi huduma na familia. Nancy Harward, Lucy Stevenson EwellVaha’i TongaVaha’i alikuwa mfano mwema kwa rafiki zake kwenye shule ya bweni kwamba waliacha kumtania kwa sababu ya yeye kusali. Hata walianza kusali na kwenda kanisani pamoja naye na wengine wakabatizwa! Sheila KindredSiri na Mambo ya kushtukizaMsichana “anamwokoa” mwanasesere wa karatasi kutoka kwenye duka na anatambua kwamba alikuwa amemuiba. Anaamua kumwambia mama yake badala ya kuiweka iwe siri. Pia anatambua tofauti iliyopo baina ya siri na jambo la kushtukiza. Jilinde MwenyeweKile ambacho watoto wanaweza kufanya na kusema ili kujilinda wenyewe dhidi ya watu na vitu vinavyowakosesha amani. Pia huwahimiza watoto kufikiria kuhusu yule wanayeweza kuzungumza naye tatizo likitokea. Kitafute!Tafuta vifaa vilivyofichwa kwenye picha. Ono la Mpango wa MunguToleo la kielelezo cha Joseph Smith na Oliver Cowdery wakipokea ono la mpango wa wokovu na kile mpango unachomaanisha kwa kila mtu duniani. Baba wa Mbinguni Ana Mpango kwa ajili YanguUkurasa wa kupaka rangi ulioandaliwa maalum kwa ajili ya watoto wadogo, uliojikita kwenye mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni. Neno la HekimaJifunze kuhusu jinsi Joseph Smith alivyopokea sheria ya Neno la Hekima. Kadi za Historia ya Kanisa Wapendwa WazaziKidokezo kwa wazazi kikiwahimiza kuwalinda watoto wao dhidi ya unyanyasaji.