2021
Chai au Sharubati ya Embe?
Julai/Agosti 2021


Chai au Sharubati ya Embe?

Mwandishi anaishi California, Marekani.

Tukio hili lilitokea huko Taiwan.

“Kwa nini hukutaka chai?” Jiro aliuliza.

“Stand for the Right,” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 159).

Picha
two boys in school uniforms walking through a market

Chung alitembea kwenye mtaa wenye shughuli nyingi huko Taiwan. Rafiki yake Jiro alikuwa karibu kando yake. Watu walikuwa kila mahali! Wanunuzi waliangalia nguo zilizouzwa, watoto walicheza michezo na watu waliharakisha kwa kuzungumza kwenye simu zao. Chung aliushikilia mkoba wake wa shule kwa nguvu kuhakikisha kuwa hakuudondosha.

“Siamini kuwa mwaka wa shule unakaribia kuisha!” Chung alisema kwa sauti ili Jiro asikie.

“Ninajua! Niko tayari kumaliza masomo,” Jiro alisema.

Chung na Jiro walipita vibanda vilivyouza aina zote za vyakula. Matunda. Pudini za matunda. Mkate wa karanga. Harufu nzuri zilikuwa kila mahali! Lakini yote ambayo Chung aliweza kufikiria ilikuwa ni jinsi alivyohisi joto.

“Ninahisi kana kwamba niko kwenye oveni!” Chung alisema.

“Mimi pia,” Jiro alisema. “Hebu tununue vinywaji.”

Walienda kwenye kibanda kinachouza vinywaji vyenye rangi.

Jiro alitoa hela. “Chai mbili za boba, tafadhali.”

Chung alijua kwamba chai ilikuwa kinyume na Neno la Hekima. “Ninaweza kupata sharubati ya embe?” aliuliza.

Jiro aligeuka kumwangalia Chung. Tumbo la Chung lilifurukuta. Je, Jiro alifikiria kwamba lilikuwa jambo la ajabu kutokunywa chai?

Mwanamke alimpa Jiro chai baridi ya boba na Chung sharubati ya embe. Kisha wavulana hao wakarudi mtaani kuelekea nyumbani kwao.

Jiro alikunywa kinywaji chake. “Kwa nini hukutaka chai? Ni tamu sana!”

Chung alilamba midomo. “Um, situmii chai.”

“Kwa nini?”

Chung alifikiria kuhusu jinsi ya kujibu swali. Wamisionari walikuwa wamemfunza kuhusu Neno la Hekima. Katika darasa lake la Msingi alikuwa amejifunza kuwa kuishi Neno la Hekima kumemsaidia kuwa na Roho Mtakatifu.

“Ninamwamini Mungu na ananitaka niutunze mwili wangu. Anaomba tusinywe chai wala kahawa wala pombe,” Chung alisema.

“Umejuaje hayo?” Jiro aliuliza.

“Nilijifunza hayo kanisani.”

Jiro alipiga funda jingine la kinywaji chake. “Hilo linaonekana jambo la upuuzi. Ni chai tu! Haitakudhuru.”

Chung alihisi kama tumbo lake lilijaa vyura wanaorukaruka. Ni vipi angemsaidia Jiro kuelewa? Labda mtu fulani kanisani angemsaidia kumwelezea Jiro.

“Ungependa twende pamoja kanisani wakati mmoja? Mimi ni mshiriki wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Unaweza kujifunza kuhusu Mungu na Yesu Kristo.”

Jiro alitafakari kwa muda mfupi. “Sidhani.”

“Sawa,” alisema Chung. Alihuzunika kidogo kuwa Jiro hakutaka kuandamana naye kanisani. Lakini bado alikuwa na furaha kwamba alishiriki ushuhuda wake.

Baadaye wiki hiyo shuleni, mwalimu wa Chung, Bwana Lin, aliomba kila mtu kuwa makini. “Kesho ndiyo siku ya mwisho ya masomo. Kwa sababu kila mtu amefanya kazi kwa bidii mwaka huu, nina zawadi. Sote tutakunywa chai ya boba!”

Wanafunzi wote darasani walishangilia. Kila mtu isipokuwa Chung. Alikaa kwenye kiti chake. Kumwambia mwalimu wake kuwa hanywi chai ingekuwa vigumu zaidi kuliko kumwambia Jiro! Kila mtu angefikiria kuwa alikuwa wa ajabu, kama vile Jiro alivyofikiria.

Picha
boy raising his hand in class

Jiro alinyosha mkono wake. “Bwana Lin? Chung hanywi chai. Ni sehemu ya dini yake. Je, anaweza kunywa sharubati ya embe badala yake?”

Bwana Lin alimgeukia Chung. “Je, hilo ni kweli, Chung?”

Chung alikubali kwa kichwa.

Bw. Lin alitabasamu. “Sawa. Nitakuagizia sharubati badala yake.”

Baada ya shule, Chung na Jiro walienda nyumbani pamoja. “Asante kwa kunisaidia,” Chung alisema.

Jiro alitabasamu. “Wewe ni rafiki yangu. Ikiwa kitu ni muhimu kwako, basi ni muhimu kwangu.”

Picha
Friend, July 2021 Tier 2

Vielelezo na Melissa Manwill

Chapisha