2021
Neno la Hekima
Julai/Agosti 2021


Hadithi za Maandiko

Neno la Hekima

Picha
Joseph Smith speaking to other members

Joseph Smith alifanya mikutano ili kuwafundisha watu kuhusu injili. Wakati mwingine wanaume walivuta na kutafuna tumbaku.

Picha
Joseph and Emma talking

Hili lilimtia wasiwasi Emma Smith. Moshi na tumbaku vilisababisha tatizo kubwa, na haikuonekana sawa. Emma na Joseph walijiuliza jinsi Mungu alivyohisi kuhusu hili.

Picha
Joseph praying

Joseph alisali na Bwana akajibu. Bwana aliwaonya waumini wa Kanisa kuhusu kuvuta sigara na tumbaku. Alisema kuwa si nzuri kwa miili yetu. Pia aliwaonya kuhusu kunywa chai, kahawa au pombe.

Picha
a pile of fruits and vegetables

Mungu alisema tule matunda, mboga za majani na vyakula vingine vyenye afya. Tunayaita mafundisho haya Neno la Hekima.

Picha
a girl eating broccoli with chopsticks

Ninaweza kuishi Neno la Hekima. Baba wa Mbinguni atanibariki ninapoutunza mwili wangu.

Vielelezo na Apryl Stott

Chapisha