2021
Marafiki Wapendwa
Julai/Agosti 2021


Marafiki Wapendwa,

Picha
Friend, July 2021 Tier 2

Kabla hamjazaliwa, mliishi na wazazi wenu wa mbinguni. Baba wa Mbinguni aliweka mpango kwa ajili yetu sote ili tuje duniani kujifunza na kukua. Huu ni mpango wa furaha. Yesu Kristo alituonyesha njia alipokuja duniani. Unapochagua kumfuata, unachagua kufuata mpango wa Baba wa Mbinguni. Unakua ili uwe kama Mwokozi!

Nenda kwenye ukurasa wa 26 ili ujifunze zaidi kuhusu mpango wa furaha. Kisha ucheze mchezo kwenye ukurasa wa 16.

Upendo,

Gazeti la Rafiki

Mahali tunaposoma Gazeti la Rafiki

Picha
two boys holding copy of the Friend

Denzel B. na Elba E., umri miaka 8 na 9, wanasoma gazeti la Rafiki kwa Kiingereza nyumbani na Kanisani huko Dar es Salaam, Tanzania.

Tunapenda Kuona Hekalu

Picha
family at the temple

Abraham, Fernando, na Enoc T., umri miaka 7, 10 na 5, walitembelea hekalu la Guadalajara Mexico pamoja na wazazi wao.

Kondoo wa Yesu

Picha
girl blowing cottonball with straw

Nilifurahia shughuli ya kupuliza kondoo kuelekea kwa Yesu kutoka kwenye mapendekezo kutoka Njoo, Unifuate (Septemba, 2020).

Ari S., umri miaka 4, Texas, Marekani

Chapisha