Kutoka kwa Urais wa Kwanza
Kuwa Mkarimu
Imetoholewa kutoka “Wazazi na Watoto,” Ensign au Liahona, Nov. 2018, 61–67.
Ninamjua kijana ambaye alikuwa mkimbizi. Kundi la vijana wengine lilimfanyia utani kwa kuwa tofauti. Walimtania kwa kuzungumza lugha tofauti. Haimfurahishi Baba wa Mbinguni tukiwa wadhalimu au wakatili kwa wengine. Ni udhalimu kumwonea mtu mwingine, kuunda kikundi ili kuwadhuru, au kuwakataa.
Watoto wapendwa, ulimwengu wetu unahitaji uzuri na upendo wenu. Kuweni wakarimu kwa kila mmoja wenu. Yesu alitufundisha kuwatendea wengine kama vile tunavyotaka tutendewe. Tunapojitahidi kuwa wakarimu, tunasogea karibu na Yeye.
Ukiwa si mkarimu kwa yeyote—mtu binafsi au kundi—fanya uamuzi sasa ubadilike. Watie moyo wengine wabadilike pia.
Nashuhudia juu ya Yesu Kristo, Mwokozi wetu, ambaye ametufundisha kupendana kama Yeye alivyotupenda. Ninaomba tufanye hivyo.
Jinsi ya Kumpata Rafiki Mpya
Je, unaonyesha vipi ukarimu kwa mtu mgeni? Vipi, ikiwa anatoka nchi tofauti? Kwa kila hatua, jaza hoja yako binafsi.
-
Tabasamu na useme hujambo.
-
“Habari! “Jina lako ni nani?”
-
“Ninafurahia kuwa uko kwenye darasa letu.”
-
________________________________
-
-
Fikiria kuhusu jinsi wanavyoweza kuhisi:
-
Aibu kwa sababu bado hawana rafiki au wanazungumza lugha tofauti.
-
Huzuni kwa sababu wamepakumbuka nyumbani kwao.
-
Wasiwasi kwa sababu ______________________.
-
-
Waalike.
-
“Je, unataka kucheza nasi?”
-
“Hebu tukae pamoja.”
-
____________________________
-
-
Kuwa mkarimu na mwenye kusaidia.
-
“Ninaweza kukuonyesha mahali pa kula chakula cha mchana.”
-
“Hiki ndicho tutakachokifanya baadaye.”
-
_______________________________
-
-
Jifunze kutoka kwao.
-
“Je, unapenda mchezo gani?”
-
“Je, unasemaje hilo kwa lugha yako?”
-
_________________________________
-
-
Ukiwaona hawatendewi ipasavyo:
-
Zungumza kwa niaba yao.
-
Zungumza nao au cheza nao.
-
____________________________
-