Onyesha na Useme
Nilimwuliza mama yangu ikiwa ningeweza kuendesha pikipiki yangu ya magurudumu matatu. Alisema ningeweza kuiendesha tu karibu na nyumbani. Nilienda mbali kidogo na nikapotea. Nilihisi hofu na kusali. Baadaye, nikatambua baadhi ya maeneo na kujua kwamba nilikuwa karibu na nyumba yangu. Ninashukuru Baba wa Mbinguni alinisaidia.
Jack S., umri miaka 9, Masovia, Poland
Nilifanya uamuzi wa kubatizwa na ninayo furaha kuwa nilifanya hivyo! Kufanya maamuzi sahihi ni muhimu.
Alicia P., umri miaka 9, Masovia, Poland
Ninajua nilikuwa nikichagua mema na kufuata mfano wa Yesu Kristo kwa kubatizwa. Nilihisi furaha na mchangamfu baadaye. Ninampenda Mwokozi wangu.
Zion M., umri miaka 9, Waikato, New Zealand
Baba yangu anamhudumia mtu asiyeona. Nilitaka kumfanyia jambo. Baba yangu alinisaidia kuweka ujumbe maalum kwenye kabati ili mtu huyo aufikie kwa vidole vyake. Ulisomeka, “Yesu anakupenda.” Nilienda na baba yangu kumpatia. Mtu huyo alistaajabu na kufurahia alipoyagusa maandishi.
Amber F., umri miaka 6, Utah, Marekani
Tulihisi kama Nefi tulipotengeneza pinde zetu.
Neil na Aaron H., umri miaka 8 na 10, Alaska, Marekani
Shule yangu ilifanya masomo kupitia mtandao kwa muda fulani kwa sababu ya COVID-19. Nilitengeneza mfano wa hekalu la Wanefi kati ya vipindi vya masomo.
Samuel J., umri miaka 9, Ohio, Marekani
Tunampenda Mwokozi wetu na tunamkumbuka daima.
Vianca na Avril V., umri miaka 10 na 6, Cundinamarca, Colombia
Meredith B., umri wa miaka 7, North Carolina, USA
“Ninapenda Kuliona Hekalu,” Clara B., umri miaka 11, Minnesota, Marekani
“Ujio wa Pili,” Santiago C., umri miaka 11, Santiago, Chile
Emerson G., umri miaka 8, Washington, Marekani