Mikono Saidizi Ulimwenguni Kote
Kutana na Eta kutoka Samoa ya Amerika
Kutana na watoto wa Msingi wakiwasaidia wengine, kama Yesu alivyofanya.
Yote kuhusu Eta
Miaka: 9
Kutoka: Samoa ya Amerika
Lugha: Kiingereza na anajifunza Kisamoa
Familia: Mama, Baba, kaka wawili na dada mmoja
Malengo na ndoto: 1) Kwenda misheni. 2) Kuolewa hekaluni. 3) Kuhitimu chuo. 4) Kurithi duka la mama yake la bidhaa za kuokwa.
Mikono Saidizi ya Eta
Mama wa Eta ana duka la bidhaa za kuokwa za kitindamlo kwenye kisiwa chao. Eta na dada yake mkubwa,Talai, wanapenda kushiriki na walimu na viongozi wao na watu ambao huenda wanapitia shida. Wakati mwingine wao huendesha gari pamoja na mama yao na kuwapa biskuti na vitafunwa vingine watu wanaowaona barabarani. Huwafanya watu kufurahia zaidi na huwafurahisha Eta na Talai kuwagawia wengine. Wanapata furaha zaidi kwa kuwagawia wengine chakula kutoka kwenye duka la uokaji kuliko kuvila wao wenyewe! Wote wawili wanajifunza kuoka kama moja ya malengo yao ya Watoto na Vijana mwaka huu, kwa hivyo wao kila mara huwa na fadhila za kuwapa wengine.
Eta anasema, “Ninapenda kushiriki na wengine kwa sababu inawafanya wao kuwa na furaha, na hunifanya mimi kuwa na furaha. Ninajua kuwa hivyo ndivyo Baba wa Mbinguni anavyotaka tufanye.“
Mambo Ayapendayo Eta
Mahali: Mabwawa kwenye kisiwa chake, ambapo anapenda kuogelea
Hadithi kuhusu Yesu: Wakati alipofufuka
Wimbo wa Msingi: “Love Is Spoken Here” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 190–91).
Chakula:Vibanzi
Rangi: Zambarau
Somo shuleni: Hisabati