2021
Yesu Alishiriki na Wengine
Julai/Agosti 2021


Kusaidia Kama Yesu

Yesu Alishiriki na Wengine

Picha
Jesus speaking to disciples on the shore

Baada Yesu kufufuka, aliwaona wanafunzi wake wakivua samaki kwenye mashua. Hawakuwa wamekamata samaki yeyote. Yesu akawaambia watupe jarife upande mwingine wa mashua. Walivua samaki wengi sana hadi nyavu zao zikawa nzito sana! Kisha wanafunzi wakaandamana na Yesu kwenye nchi kavu. Walikaa Naye kando ya moto. Yesu alishiriki mkate na samaki pamoja nao. Alimwuliza Petro, “Je, unanipenda?” Kisha akasema “Lisha kondoo wangu.” Hiyo inamaanisha kwamba alimtaka Petro kushiriki injili pamoja na wengine. Tunaweza kuonyesha upendo kwa Yesu kwa kushiriki na wengine, kama Alivyofanya.

Picha
A photo of Grayson Copa

Nilisaidia kutengeneza biskuti kwa ajili ya jirani zetu wageni. Mwanamke alizungumza Kiarabu tu, lakini alitualika ndani. Tulikaa pamoja na kufahamiana hata ingawa hatukuzungumza lugha moja. Alikuwa mkarimu sana, na ilinifanya nihisi vizuri ndani.

Grayson C., umri wa miaka 5, Abu Dhabi, Muungano wa Falme za Kiarabu

Picha
Friend, July 2021 Tier 2

Kielelezo na Kamille Corry

Chapisha