2021
Jilinde Mwenyewe
Julai/Agosti 2021


Jilinde Mwenyewe

a boy standing in front of road signs

Unapaswa kuwatendea watoto wote wa Baba wa Mbinguni kwa ukarimu na heshima. Pia unapaswa kutarajia wengine wakutendee vivyo hivyo. Mtu akijaribu kukudhuru kwa maneno au vitendo, si SAWA!

Ikiwa unahisi kuwa hauko salama …

  1. Sema hapana.Huhitajiki kufanya chochote unachohisi kuwa si sahihi au kinachokukosesha amani. Ni SAWA kusema hapana.

  2. Sikiliza hisia zako. Roho Mtakatifu anatupa maonyo tulivu ya kutusaidia kuwa salama. Ikiwa unahisi kuwa kuna tatizo, usishiriki na jaribu kuondoka ukiweza.

  3. Usitunze siri za kuumiza. Kuna tofauti kati ya jambo la kushtukiza la furaha na siri ya kuumiza. Hupaswi kamwe kutunza siri ya kuumiza, hata ikiwa uliahidi.

  4. Mwambie mtu mzima unayemwamini. Jambo baya likitendeka au ukihisi woga, mwambie mtu anayeweza kukusaidia moja kwa moja, kama vile mzazi, mwalimu, au kiongozi wa Kanisa.

Je, ni nani unayeweza kuzungumza naye ukiwa na tatizo? Andika orodha ya watu wa kuaminika hapa:

Vielelezo na Jennifer Bricking