2010–2019
Uhudumiaji
Aprili 2018


2:3

Uhudumiaji

Tuta mfumotekeleza mfumo mpya, mtakatifu wa kutunza na kuhudumia wengine.

Asaanteni, Mzee Gong na Mzee Saores, kwa kuonyesha imani ya moyoni mwenu. Tunashukuru sana kwa ajili yenu na wenzi wenu.

Kina kaka na kina dada wapendwa, sisi kila mara tunatafuta maelekezo kutoka kwa Bwana juu ya jinsi tunaweza kuwasaidia waumini wetu kushika amri za Mungu, hasa zile amri mbili kuu za kumpenda Mungu na majirani zetu.1

Kwa miezi tumekuwa tukitafuta njia bora za kuhudumia mahitaji ya kiroho na ya kimwili ya watu wetu katika njia ya Mwokozi.

Tumefanya maamuzi ya kutahafisha ufundishaji wa nyumbani na utembeleaji kama tunavyojua. Badala yake, tutatekeleza mfumo mpya, mtakatifu kwa kutunza na kuhudumia wengine. Tutaziita juhudi hizi kwa urahisi kama “kuhudumu.”

Juhudi za ufanisi za kuhudumu zinawezeshwa na vipawa vya asili vya kina sasa na kwa nguvu za ukuhani zisizo na kifani. Sisi wote tunahitaji ulinzi kutoka kwa hila za ujanja za adui.

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na Dada Jean B. Bingham, Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, wataeleza jinsi jinsi ndugu wa ukuhani waliopangiwa na kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama waliopangiwa na Wasichana sasa watafanya kazi katika kuhudumia na kutunza waumini wa Kanisa kote ulimwenguni.

Urais wa Kwanza na Kumi na Wawili umeungana katika kuidhinisha ujumbe wao. Kwa shukrani na kwa maombi tunafungua sura mpya katika historia ya Kanisa. Katika jina la Yesu Kristo, amina.